-->

Header Ads

KISIWA CHA ZUNIGA (9)

 

Na Adalgisa Kweka

Salu aliitoa mikono ya mzawa Luka nakukimbia kiasi cha kumshtua hata mlinzi aliyekuwa pale nje alishtushwa na mbio kiasi chakumfanya aende ofisini kwa mzawa kuhakikisha kama ni mzima maana mbio za Salu zilifanania za muaji.
"salama?" aliuliza baada yakumkuta mzawa Lucas tiyari amesimama mkono wake kulia ukiwa kichwani mwingine ukishikilia Meza Yake.
"ooh!salama kabisa hakuna tatizo" hili lilikuwa picha la kihindi lenye chumvi nyingi kuzidi uongo.
Salu alinyoosha moja kwa moja kwenda kwenye chumba chake ambako alikuwa mwenyewe tu kwani koku alishaimaliza safari Yake. Alipofika chumbani kwake alifunga mlango nakujirusha kitandani kwake akitafakari maneno ya mzawa yule Kisha akakumbuka stori ya mjamzito aliyopewa na Tuli aliiona ndipo alipokuwa akielekea endapo atayaruhusu yatokeee hata hivyo hakuwa na uwezo wakuyazuia yasitokeee. Mawazo hayo yalimfanya apitiwe na usingizi.
Kwa upande wa Tuli alishtuka nakujikuta yupo wodini aliinuka ijapo kuwa kwa shida nakuangaza huku na kule ambapo aliwaona wagonjwa wengine alipoiangalia miguu yake aliiona imepungua kidogo.
"He-ey! (wewe)" ilikuwa sautI iliyotoka pembeni yake ambayo ilionyesha hali ya uchovu, Tuli aligeuka upande wa kulia nakumuona kijana mwenzie aliyekuwa amelala huku akigeukia upande wa Tuli.
"hey"Tuli alimrudishia salamu huku bado akimtafakari alikuwa ni nani.
"pole" alimpa pole Tuli kitu kilichomshangaza sana Tuli kwani wote walikuwa wagonjwa.
"Asante pole na wewe"alimwambia mwenyeji mwenzie ambaye alikuwa na huzuni tele, Tuli alirudi kujilaza kwani miguu yake ilimuuma lakini alimgeukia yule mwenzie raundi hii, wote walikuwa wakiangaliana huku macho yao yakiwa yanatoa ushahidi wa misukosuko ya kisiwa.
"marehemu alikuwa anaitwa Gorge, alikutana na Lisa hapa kisiwani, walipendana ingawa sikuwashuhudia but I could see it in his eyes and from each words that came out from his mouth (lakini niliweza kuliona hilo kwenye macho na katika maneno yaliyo toka kinywani mwake. Alimpenda lisa sana their story made me believe love was possible in Zuniga even though it was something I never think of. (stori yao ilinifanya niamini kuwa mapenzi yaliwezekana katika kisiwa cha Zuniga ijapokuwa mapenzi ni kitu ambacho sijawahi kukifikiria)" mwenyeji yule alitabasamu licha yakwamba stori hyo ilimuumiza pia kwa ndani.
"Lisa alijua kuwa anamimba akamjuza Gorge ambaye akaona bora watoroke jambo ambalo lilileta balaa, Lisa ndiye aliyemuua mzawa but who would believe his story other than us (lakini nani angemuamini Gorge zaidi ya sisi)" ilikuwa ni ukweli usiopingika kuwa wazawa wasiingemuamini Gorge labda wenyeji wenzie.
"If Lisa couldn't do it then Gorge could have done (kama Lisa asingemuua yule mzawa basi Gorge angemua)"baada yakuwa msikilizaji sana Tuli aliongezea mawazo yake ambayo yalikuwa sahihi kabisa.
"ndyo na amekufa and am  happy (nimefurahi) kwani hiko ndicho alichokihitaji, alishapoteza Tumaini lake"
"maskini Gorge" Tuli alimsikitikia sana.
"nikikitafakari hiki kisiwa sikimalizi.. Kiko wapi? Kimezungukwa na nini? Wazawa wametoka wapi?.. I don't know I only know one thing forsure that I will die one day so am going to enjoy life (sijui,najua kitu Kimoja kwamba Siku moja ntakufa hivyo basi nataka nifurahie maisha" aliyasema ya moyoni ambayo yalimshtua Tuli ambaye hakuwa amekubali kifo kirahisi hivyo.
"labda tutapata nafasi kilio chetu kitasikika, milango itafunguliwa" alijitahidi kumsaidia mwenyeji Mwenzie huyo ilimradi arudishe Tumaini.
"hakuna hiko kitu hapa kibaya zaidi hiki kisiwa chote kipo chini ya mheshimiwa-"
"shhhshh"alimuwahi kabla hajamalizia kwakumwambia anyamaze. Kwani uzito wa jambo hilo si mdogo na adhabu yake ni kifo ambacho walifaulu KukikwepA mahabusu hivyo ilibdi waifunge midomo Yao.
"kisiwa cha Zuniga" aliongea kwa kebehi utafikiri Kulikuwa na mzawa karibu atakayemuona.
"KISIWA KISICHOFIKIRIKA"tuli alimalizia.
Wakiwa kimya walisikia mlango ukifunguliwa wote walijifanya wamelala kana kwamba hawakuamka.
"Tuli na Mary"walishangaa kusikia majina yao yakiitwa. Walijifanya ndo wanaamka Muda wote Tuli hakujua kuwa aliekuwa anaongea naye aliitwa Mary kwani visa vya kisiwa viliwachanganya akili .hawakuweza kujifanyisha kwasasa hivyo waliamka ndipo Tuli alipomuona yule mkuu.
"habari zenu" Alilwasalimu alikuwa tofauti na wale wazawa wengine wote si kimuonekano tu bali hata tabia na alikuwa haonekani Mara nyingi.
"nzuri mzawa"waliitikia kwa pamoja.
"Mary uko vizuri kwa sasa unaweza ukarudi kwenye kitengo chako ila Tuli utaondoka jumapili" alimaliza kusema kilichomleta nakuanza kuondoka ila alirudi nakugeuka kama amesahau kitu huku wakina Mary wakimuangalia tu.
"KISIWA HIKI NI KAMA BINADAMU KINA MACHO, MASIKIO NA VIUNGO VYOTE KASORO KIMOJA HAKINA MOYO WA BINADAMU" aligeuka nakuendelea na safari huku Tuli na Mary wakibaki wanamshangaa wasielewee chochote. Alishampoteza Tuli alivyomwambia ataondoka jumapili wakat hata hakujua Leo NI siku gani.
"mmh bila shaka aliyasikia mazungumzo yetu" alionekana kupata jibu la tafakari yake juu ya maneno ya mkuu.
"Mary shsh bado wanatusikiliza" alimwambia hakujua kama ni mtu mmoja anawasikiliza au jopo la watu. Kesi yake ya mauaji hakuelewa kama imeisha ila hakutaka kesi nyingine tena. Aliamua kupumzika huku akitafakari maneno ya mkuu wa kitengo cha afya.
"MWENYEJI MARY" ilikuwa sauti ya mzawa ikimuita mary ambaye aliitikia nakuinuka kutoka kitandani kwake nakushuka hakuwa anaumwa hata kidogo zaidi yakuigiza ilikuepuka hukumu ya kifo. Alimuaga Tuli ni kama hawakujua watakutana lini na wapi inawezekana wasikutane milele maanke kisiwa hakielweki.
"kama hatutokutana tena I want you to know that meeting you was a blessing (nahitaji ujue kuwa kukutana na wewe ilikuwa ni Baraka Tosha)"
"mimi pia"alimsindikiza kwa macho, duniani watu walikumbatiana wakiagana lakini Zuniga haikuwepo hiyo. Zuniga ni ulimwengu mwingine tofauti na wakibinadamu Kuna majengo mazuri na mahitaji yote muhimu kwa binadamu kasoro yake ni moja nayo ni kila aliyeingia humo hakutoka akiwa Hai. Siri ya nani mwenye nguvu kubwa katika hiko kisiwa ilikuwa kwenye mioyo ya watu wawili mmoja akiwa Mary na Mwingine Tuli,ni Siri ambayo walitakiwa wafe nayo hata wakibahatika kutoroka nakurudi mwakao nani angewaamini wakimsingizia raisi katika issue kubwa hivyo hawakuwa na ushahidi wowote zaidi ya miili Yao iliyochoka,wangeweza kuambiwa ni wasaliti waliokuja kuharibu nchi kwani walishachukuliwa kama wafu Makawao. Watu husema hakuna siri ya watu wawili ila ZUNIGA ipo siri Kati ya watu tena zaidi ya wawili.
********************************************************************************** MIEZI 8 BAADAE.. Saluat alikuwa ashaanza kufanya kazi kwenye shamba la mhandeni, kila siku aliliona jipya lilikuwa ni gumu kama mzawa Luka alivyomhusia,alikuzoeleka hata kidogo Lilishamtia vidonda vyakutosha lakini licha ya yote hayo hawakubahatika kukipata walichokifuata jambo hili liliwakatisha tamaa sanaa walitamani waache kitengo hiko ila walishindwa;ni kama walijuta lakini hawakutaka kuonyesha. Kwa upande wa Tuli alishazoea kitengo chake licha ya magumu yote aliyoyapitia huku kesi ya mauaji ikifutwa kutokana na ushahidi kutokujitosheleza. Licha ya matatizo yote bado kulikuwa na jambo linalomsumbua na hili silingine zaidi ya LA mkuu wa kitengo cha afya hakumuelewa kabisa alikuwa akimjali sana kiasi chakuhisi Kuna kitu anataka hakuwa na mtu wakuongea naye ijapokuwa alizoeana na baadhi ya watu ila hakuweza kuwaambia yaliyomo moyoni mwake. Bado hakusitisha mpango wake wakutoroka hata kidogo aliamini ipo njia ijapokuwa hakujua hiyo njia ataigundua lini licha ya vifo vinavyongezeka kila siku. *************_________________******************__________________**************** Tarehe 25/12 ilikuwa siku nzuri sana duniani lakini kwa kisiwa haikujulikana kwani hawakujua ni Tarehe gani au lini labda watu WA kitengo cha kiteknolojia. Ila taarifa zilisambazwa kuwa kutakuwa na ugeni Kisiwani hivyo kila mwenyeji alitakiwa awe katika sehemu yake. Hawakuwajua hao wageni ni kina nani wanatoka wapi na wanakuja kufanya nini ila walichojua wao ni kwamba hawakuwa tofauti na wazawa waliowakuta kisiwani Zuniga. Salu alikuwa yuko Hoi kitandani kwake, hajiwezi kabisa, alikuwa amechoka mithili ya trekta. Ghafla mlango wake ulifunguliwa kwani alivyoingia hakukumbuka kufunga mlango kutokana na uchovu. Ndani ya miezi nane alibadilika sana hakuwa Salu yule aliyefika Mara ya kwanza kisiwani alikonda licha ya lishe nzito anayoipata kisiwani, alifubaa licha ya maji kuwepo kwa wingi tena katika bafu za kisasa kwakweli mtu akiletwa kutalii kisiwani Zuniga asingeelewa kwanini watu wameisha, wanatamani kufa na sura zao zimesusia tabasamu nakuamua kuvunja mkataba na furaha kabisa. "Saluu" aliita. Saluat alijua watu watatu ambao hupendelea kumuita hivyo nao ni Tuli ambaye hakuonana naye miezi saba tiyari alishahisi amekufa kama koku, Victor ambaye yuko naye kwenye shamba la mhandeni na WA mwisho ni Malaika wake WA kisiwani mzawa Luka ambaye alitaka kumuonyesha kuwa mapenzi kisiwani tena Kati ya mzawa na mwenyeji ambaye ni marehemu mtarajiwa yanawezekana. Ndiyo yanawezekana ila watakuwa wanakutana wapi? Atafaidi nini?vipi mimba ikija katikati itakuwaje? Kwakweli ya kaizari aachiwe kaizari ila ya ngoswe akaulizwe majaliwa tena bila nduguze kujua. "Saluu"alimuita tena, mara hii alimsogelea mahali alipofika aliketi karibu na uso wake ulionyesha Hali ya mchoko uliopitiliza ukimsogelea karibu unaweza muhisi chokoraa si kwa mavazi au uchafu Bali sura ilivyobabuka na kumsinyaa kama kikongwe. Saluu alitingisha kichwa kuashiria anamsikia masikini Saluat Zuniga ilimnyonya nguvu zake zote haikumuacha na za akiba zaidi ya zile zilizomuwezesha kufika chumbani kwake. "pole" alimpa pole hii ilikuwa kawaida yake Sasa, salu alimtingishia kichwa kuashiria ameikubali pole Ile hii ndo ilikuwa zungumza yake Leo. "Salu nilikuhisi usiende mihandeni nilijua-" "Luka una simu?" alimkatisha, ila jinsi alivyomuita mzawa Luka kwa Jina Lake ilimshtua mzawa yule asijue nini kimemfika Leo lakini chaajabu zaidi ni Salu kumuuliza kuhusu simu ni kitu ambacho hajawahi muuliza,hvyo mpaka leo anamuuliza kulikuwa Kuna kitu hakujua ni nini ila alihitaji kujua. "Ipo lakin-" "nikimpigia simu mama yangu atanielewa? Atanisaidia? Atanisikiliza?atajua mateso yangu bila kuniona? Hivi ataniamini? Na akiamua kunisaidia atanisaidiaje? Akiingia kwenye mitandao atapata maelezo ya hiki kisiwa kweli? Jamii itamuelewa akijaribu kupaaza sauti, itashirikiana naye kweli? Vipi serikali itamuelewa kweli licha ya kwamba wauaji wametoka humo? Au kama ilivyo hukumu ya kisiwa basi mama yangu atauliwa.. Ee Zunigaa"alitoa maneno yaliyojeruhi moyo wa mzawa Luka hata hvyo maneno Yale yalikuwa kama vichomi vilivyokosa tiba mbadala hivyo kumtesa kila siku . "saluu-"alikatishwa tena "wewee unamajibu ya maswali yangu na mimi nataka unijibu maswali yote" alimbadilishia kibao tena aliinuka nakuketi vizuri. "mimi!"kweli alishtuka aliona saluat WA leo si yule wasikuzote. "NDYO WEWE!"aliongea mithili ya mzawa huku jasho jembamba likimtoka kwa pembeni. "Salu una nini leo?"hakumuelewa mwanamke huyu aliyetokea kumpenda bila sababu ya msingi. "NATAKA MAJIBU"aliongea kwa ukali sasa hivi "Sawa NDYO MAMA YAKO ATAKUFA!!kwahyo kama unataka kutoroka, toroka huku ukijua uko mwenyewe usiwahusishe watu wa nje kwani kisiwa kipo kama binadamu kina masikio, mdomo na vinginevyo kasoro ni moja hakina moyo wa kibinadamu kwa mtu YEYOTE" Alitilia mkazo, Salu alinyong'onyea machozi yalimtoka sasa aliona ni jinsi gani ilikuwa mbinde kwa watu kufanikiwa kutoroka kisiwani humo. "Kwanini lakini, Kwanini? Kwanini mnatufanyia hivi" alisema saluat huku akimpiga luka kifuani, luka aliishika mikono ya saluat Kisha akainuka. "Leo hauko vizuri, ukiwa vizuri unajua wapi pakunipata" alimuachia mikono nakuondoka. Saluat alirudi kulala huku akilia kwa huzuni Sana,ndoto zakutoroka zilishaanza kupotea taratibu aliona bora koku aliyekufa kuliko yeye anayesubiria siku yake itakapofika. Aliwaza sana mpaka kichwa kikamuuma, alipoamua kuinuka hapo kichwani alisikia sauti ya mzawa ikiashiria Muda wa kula, saluat aliinuka nakutoka nje ya jengo la kulala kisha aliendelea mpaka alipofika kwa mlinzi ambaye alipoiona sura ya salu alimuachia apite. Alitembea mpaka kwenye ofisi ya mzawa Lukas alipofika aliingia bila hodi Kisha aliufunga ule mlango nakumfuata Lukas ambaye alikuwa amesimama akimshangaa saluat Muda wote alihisi Kuna kitu kimemuingia kichwani leo "Luka naomba unisaidie nitoroke" alimuomba ombi ambalo Hajawahi kuombwa na kijana au mwenyeji yeyote yule. "salu.."alihisi amesikia vibaya ila saluat alipiga magoti nakuushika mkono wa mzawa luka kuonyesha anamaanisha anachokisema. "nakuomba" alikuwa analia "salu HAPANA... HAPANA!!!!"alisema huku akiutoa mkono wake mikononi mwake,saluat aliendelea kuomba tu,akiamini kwa Masada WA upendo alionao mzawa huyo kwake angemsaidia. "Salu,mimi nikusaidie utoroke afu mimi unaniacha na nani?" swali lile lilimchosha salu aliona ombi Lake lilishakataliwa alikilaumu kichwa chake kwakuto kufikiria. "Kama unanipenda hutotaka niteseke" alitafuta Gia zakumuingia mzawa luka. "nakupenda ndomana nikakwambia usiende katika shamba la mhandeni! Ila hukunisikiliza matokeo yake ndo haya" alimpa ukweli usiopongika. "nakuomba" alizidi kumuomba "Salu nitakusaidia endapo ukinisaidia pia, sitaki utoroke hapa kama salu nataka utoroke hapa kama mpenzi wa luka tena tutoroke wote na sivinginevyo..." aliyatoa ya moyoni Saluat alibaki mdomo wazi..... ITAENDELEA..

Powered by Blogger.