-->

Header Ads

Mwandishi Guardian aokotwa akiwa hajitambui

Mwandishi na mhariri wa Dawati la Biashara wa Gazeti la The Guardian,  FINNIGAN SIMBEYE ameokotwa akiwa hajitambui katika eneo la Bunju jijini Dar es Salaam ambapo kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hosipital ya Wilaya ya Kinondoni ya Mwananyamala.
Mke wa mwandishi huyo, Rosemary Mirondi amesema anamshukuru Mungu kutokana na mumewe kumtambua baada ya kumuona katika Hospitali ya Mwananyamala ambapo muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema mwandishi huyo anaendelea na matibabu zaidi.
Mapema asubuhi ya leo, Jumapili Aprili  8 kulizagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kuokotwa kwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la The Guardian maeneo ya Bunju.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Gazeti la The Guardian amesema Kampuni imepokea kwa mshituko tukio hilo la mfanyakazi wao na wanaamini kuwa uchunguzi utafanyika kuweza kufahamu kilichomtokea mwenzao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, RPC Mlilo  amethibitisha kupokea taarifa hizo  baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu.
Mke wa mwandishi huyo pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya The Guardian wote kwa pamoja wanasema wanaendelea kusubiri ripoti ya madaktari na polisi juu ya tukio hilo la kujeruhiwa na kuokotwa kwa mwandishi na mhariri huyo wa gazeti la The Guardian.

No comments

Powered by Blogger.