Bill Nas aijibu kauli ya Dayna Nyange kuwa mastaa wa Kibongo hawajui kutongoza
Bill Nas ameijibu kauli ya Dayna Nyange kuwa mastaa wa Kibongo hawajui kutongoza.
Dayna aliiambia Bongo5 kuwa hiyo ndio sababu moja wapo ya kwanini hana uhusiano na staa mwenzake. Lakini Bill ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo wa Dayna, Komela, ameipinga vikali kauli hiyo.
“Hapaswi kujumuisha wasanii wote wa Bongo Flava, kama kuna washkaji wawili watatu wamewahi kumtongoza au watano, bado umma wa Bongo Flava ni mkubwa sana,” Bill Nas alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Jumatano hii.
“Kama kuna watu wawili watatu, aseme hao hao asijumuishe watu wengine,” ameongeza rapper huyo na kudai kuwa kwakuwa yeye hajawahi kutoka na msichana wa Bongo Flava, hawezi kuhitimisha kuwa hakuna msichana anayemvutia.
Awali kwenye interview ya Bongo5, Dayna alisema, “”Sijawahi kudate na staa na si kwamba wakaka wazuri hawapo, na sio kwamba hawanitokei, labda hawajui kutongoza vizuri. Kwa sababu sijawahi kushawishika kutembea na staa na sipendi kutembea na staa, so wakati mwingine unaweza ukawa haupendi kitu lakini ukashawishika kuingia lakini mimi bado hajatokea.
No comments