-->

Header Ads

Cassim Mganga: Nilifuta verse yangu kwenye ‘Somo’ baada ya kusikia alichoimba Nyota

Cassim Mganga ni fundi haswaaa kwenye uimbaji, lakini hivi karibuni amekiri kukutana na fundi mkongwe, Nyota Waziri wa Kilimanjaro Band, Wana Njenje aliyemshirikisha kwenye wimbo wake, Somo.

Cassim ameiambia TOVUTI YA Bongo5 kuwa alilazimika kufuta na kurudia sauti zake kwenye wimbo huo alizoingiza kwanza, baada ya kusikia kile alichoimba Nyota kwenye wimbo huo.
“Mimi nilirudi kufuta verse yangu,” anasema Cassim. “Maake unajua mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kurekodi nikatoka nje, nimekaa nje namsikia mama anaimba ndani, nikaingia ndani nikamwambia ‘mama nafuta’, watu walicheka sana. Nikamuambia ‘mama nafuta, siwezi kukubali namna hii.’
“Nyota ni mwanamuziki kwa kifupi, legend, mtu ambaye anazeeka na sanaa yake, mtu ambaye anazeeka na uwezo wake. Mimi ni shabiki mkubwa wa Nyota, nimefurahi sana kufanya naye kazi yaani inakuwa kama nimeitimiza ndoto yangu,” amesisitiza Cassim.
Utazame wimbo huo hapo chini.

No comments

Powered by Blogger.