-->

Header Ads

Video: Lulu Diva azungumzia tuhuma za kuhusika na biashara ya dawa za kulevya

Lulu Diva, mrembo anayefanya muziki wa Bongo Flava ambaye alitajwa kwenye orodha ya watu wanaodaiwa kuhusika na madawa ya kulevya amezungumzia alivyochukulia na jinsi wazazi wake walivyojisikia.
Akiongea na Bongo5, mrembo huyo amesema hakutarajia kutajwa kwenye orodha hiyo na ni kitu ambacho kiliwashtua mpaka ndugu zake kwa kuwa hajawahi kujihusisha na biashara hiyo haramu.
“Nilishtuka kwa sababu ni kitu ambacho sikuwahi kutarajia wala kutegemea kwa kuwa nilikuwa sifahamu chochote. Nilivyosikia vile nilikosa raha kabisa niliumia lakini namshukuru Mungu by the way,” amesema.
“Bado inaniaffect kwa kuwa ni itu ambacho hujawahi kutegemea, huhusiki wala hujawahi kufanya kwa hiyo kitu kama kile kinakuumiza pale unapokuwa unakutana na watu ambao hawafahamu halafu huwezi kusema unamkalisha mtu uanze kumpa somo umuelezee,” ameongeza.
Lulu amedai kuwa mpaka leo hii taarifa za tukio hilo hazijaweza kumfikia mama yeke kwa kuwa yupo mbali ambaye anaishi mkoani Tanga na kipindi alikuwa anajua mwanae kasafiri kwakuwa alishamuaga tangu muda mrefu.
“Mama yangu mpaka leo hakuwahi kufahamu kwa sababu the time niliyokuwa nimetajwa nilikuwa natarajia kusafiri kwahiyo akawa anajua mimi nimesafiri. Na vile kwa sababu yupo mbali hakuwahi kupata taarifa mapema lakini kwa ndugu zangu ndio iliniaffect sana kwa sababu wenyewe pia wanashangaa kwa sababu wapo na mimi muda mwingi na wanajua jinsi walivyonikuza na wananielewa vizuri mtoto wao. Kwa hiyo ilikuwa pia surprise na waliangalia vitu vingi kwa wao wenyewe kwa baadhi ya watu kuwalaumu.”
Kuhusu kulala rumande kwa siku tano, Lulu amesema, “Kipindi kile mule ndani sikuhitaji rafiki, yaani nilikuwa nasali nakesha nikiomba Mungu ili ukweli ujulikane ili nije kutoka mule ndani,” amesema

chanzo: BONGO5

No comments

Powered by Blogger.