Wanafunzi 8000 hatarini kufutiwa udahili vyuo vikuu
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema zaidi ya wanafunzi 8,000 wa vyuo vikuu 52 nchini wapo njia panda ya kuendelea na masomo baada ya uhakiki kukamilika.
TCU ilitoa taarifa yake Jumatano hii kwa vyombo vya habari, kuwa imewabaini wanafunzi ambao wamedahiliwa katika programu ambazo hawana sifa. Orodha ya wanafunzi hao tayari imewasilishwa kwenye vyuo vikuu vya Dar es Salaam (UDSM), Dodoma (UDOM), Mtakatifu Augustine (SAUTI) na Tumaini.
Aidha taarifa hiyo imebainisha kuwa orodha ya wanafunzi wasio na sifa imeshawasilishwa kwenye vyuo husika.”Hivyo wanafunzi wote wanaoendelea na masomo kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini wanaweza kutazama matokeo ya uhakiki wao kupitia tovuti ya tume,” ilisema taarifa hiyo kupitia tovuti ya tume hiyo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alilotoa mwaka jana, mwezi Agosti baada ya kutangaza kuwapo kwa wanafunzi ‘hewa’ ambao wanapatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
CHANZO; BONGO5
No comments