-->

Header Ads

ENYI WANASIASA SOMENI SHAIRI HILI

Image result for ndugai vs zitto



 ULIMI
Ulimi nyama laini, sumu iuayo sana
Wengi wako hatarini, amaniyo yagongana
Hofu i tele moyoni, dunia yasalitiana
Ulimi kitu kidogo, chaangusha hata Dunia

Machafuko mitaani,vijana watadundana
Neno latoka mdomoni,gonjwa linaoteana
Lakomaa hadi ndani,visasi vya zaliana
Ulimi kitu kidogo,chaangusha hata Dunia

Ulimi hata chumbani, wazazi hutifuana
Maneno ya mitaani,yaingiapo chembana
Heshima 'dondoka chini,kwenye ndoa hutengana
Ulimi kitu kidogo, chaangusha hata Dunia

Ulimi nyama laini, laua hata Dubwana
Giza tete maishani,amani kama Dafina
Imejizika ardhini, magomvi ni yake mnuna
Ulimi ni sumu kali,inayoua taratibu







Diwani ya Mea

No comments

Powered by Blogger.