-->

Header Ads

KISIWA CHA ZUNIGA (8)

 

Na Adalgisa Kweka.

"noo(hapana)" alikataa katakata licha yakwamba ukweli ulikuwa ushagundulika.
"Tuli, kisiwa hiki kina masikio kila sehemu" alishamchoma sindano Tuli wakati anamwambia hayo ulikuwa kitendo cha ghafla tu.
"Mkuu mim-"hakumalizia alichotaka Sema macho yalifunga ghafla sindano aliyomchoma ilikuwa kali sana. Mkuu wa kitengo alibaki anamuangalia Tuli ambaye alikuwa ameshalala, Tuli alikuwa mrembo sana ila matukio aliyokumbana nayo kwenye kisiwa cha zuniga yalimfanya afubae na urembo wake ufifie. Mkuu yule aliweka mkono wake wa kulia kwenye shavu la Tuli na kama haitoshi aliusogeza mkono wake maeneo yote ya usoni kisha alizishika nywele za Tuli zilizokuwa zimekakamaa kuashiria zmekosa mafuta, alimuangalia Tuli kwa muda mrefu bila kusema neno Kisha aliutoa mkono wake.
"mzawa!!"aliita sekunde chache mzawa alikuwa ashaingia ndani kwa mkuu.
"mchukue mpeleke wodini, utawapa hiki" alimkabidhi kikaratasi.
"Sawa mkuu"Aliitikia wito nakumbeba Tuli Kisha kuondoka naye, alipofika wodini walimpokea nakumlaza kitandani Kisha aliwapa kikaratasi alichopewa na mkuu wa Afya.
********************************************************
Sauti ya mlango kugongwa ilimshtua saluat aliyekuwa amelala usingizi wa pono. Aliamka ndipo alipogundua kuwa Tuli hakuwepo moja kwa moja akajua aliyekuwa akigonga mlango ni Tuli, lakini akili Yake ilipinga kwani alijiuliza Tuli atafungaje mlango? Alipoangalia kwenye kitasa aliona funguo iko palepale hivyo alijua mgongaji si Tuli. Aliinuka na kwenda kufungua mlango, alikutana uso kwa uso na mzawa malaika kama alivyopenda kumdhania, mikononi mwake alikuwa amebeba Chai na vitafunwa.
"unaendeleaje Salu"hakuongea kizawa tofauti na siku zote hizo.
"vizuri, karibu"alimkaribisha kiukarimu kama yupo kwao. Mzawa yule aliingia ndani nakuketi kwenye kiti.
"pole"
"Asante nashukuru mzma now"alijisahau mazungumzo Yao yalikuwa kama ya watu wawili wanaofahamiana siku nyingi.
"vizuri"aliona aivunje Mada aliyokuwa anaongelea
"unahitajika kazini sasa hivi" alimwambia kilichomleta hapo.
"ndyo mzawa ila-"alisita kidogo alitaka kumuuliza juu ya Tuli alitaka kujua kama mzawa yule anajua chochote." Tuli sijamuona umemuona huko? "alijikaza nakuuliza.
"Tuli"alilitaja Jina kana kwamba analisikia kwa mara ya kwanza." Tuli yuko mahabusu "alimwambia bila kusita.
"mahabusu!"alishangaa ameenda kufanya nini Huko? Alijiuliza maswali yasiyo na Malibu.
"Kuna mjamzito amefariki na-"
PPM "hajaua Tuli wangu jamani" alisikitika sana hakutoa chozi kutokana na mbavu 1kumuuma sana.
"NAKUSIBIRIA NJE UNADAKIKA TANO!"alibadilika kutoka kwa mzawa Malaika kuwakama wazawa wengine
"Sawa mzawa"aliitikia. Mzawa aliondoka nakumuacha saluat akijiandaa, hakuchukua muda alikuwa tiyari.alitoka nje ambapo kwenye korido alitembea huku na huku akipishana na vitanda vitupu alipofika Mbele alikuta mjamzito mmoja akiwa amelala, alimuangalia Kisha alitoka nje ndipo alipomkuta mzawa yule akimsubiri.waliendelea na safari walikuwa wakielekea shambani.
"Naitwa Saluat" alijitambulisha Kam hajulikani lakini alikuwa na dhumuni lake moyoni ambalo hakujua kama litatimia.
"Mzawa Luka"alijitambulisha bila uwoga huku safari ikiendelea kama kawaida. Safari ilijaa ukimya sana kiasi chakutia uvivu.
"Tuli watamfanyeje?" aliuliza hili lilikuwa la msingi sana kuliko chochote.
"sijajua ila amehukumiwa kwa kesi ya mauaji" alikuwa anafanya makosa lakini hakusita aliendelea.
"watamuua kweli" aliuliza alihitaji kujua hatima ya rafiki yake mpenzi.
"ushahidi ukiwekwa mezani"
"Tuli si mauaji" aliendelea kumtetea licha  yakwamba sauti yake isingefika popote.
"KISIWA CHA ZUNIGA KINA SIRI NYINGI AMBAZO HUTAKIWI KUZIJUA" alimsisitizia Saluat ambapo akili zilimrudia nakumfanya akumbuke Kuwa yupo kisiwani Zuniga tena pamoja na mzawa.
"KISIWA hiki kiko wapi?"aliuliza kana kwamba hakuelewa kauli ya mzawa Luka.
"Salu, uko tiyari Kufa?" alimuuliza swali lililomshtua sana.
"ha-p-a-na"aliongea kwa uwoga.
"siwez jibu swali lako" lilikuwa jibu linaloeleweka na lilizimisha stori zao zote,kimya kilitawala mpaka wanafika shambani ambapo salu alijichanganya na watu Kisha akaanza kufanya kazi. Muda wote huo hata hakufikiria kuhusu Victor kabisa. Kazi za shambani zilipamba moto ukichanganya na juakali walikuwa Hoi kabisa, Kazi hiyo haikuwa na mapumziko Kwani wazawa waliowasimamia walikuwa wamebeba mitutu iliyoogopesha.
"salu" ilikuwa sauti ambyo si ngeni ilimuita. Salu aligeuka nakumuona Victor ambaye alimpa ishara yakuendelea na Kazi, Victor alikuja kusimama pembeni yake huku Kazi ikiendelea, Victor alikuwa akilima huku salu aking'oa majani kwa mikono yake licha yakuchanwa na majani.
"Tuli yuko afya ni mzima" alidanganya ilikuwa heri kusema uongo kuliko ukweli ambao ungewavunja moyo.
"Inshallah!! Ndo umefika shambani Mara -"
"ndyo" alishajua alichotaka kumuuliza
"Huku ni kifo tu"kauli yake ilimshtua sana salu ambaye neno kifo alishalisikia kisiwani mara nyingi.
"kwanini"
"sheria ngumu, ukionekana umesimama tu ufanyi Kaz,umechoka au unaumwa unapigwa shaba" salu aliuziba mdomo wake kuonyesha aamini hayo yanayosemwa.
"jana mwenzetu moja kauliwa mbele yetu daah hawa si watu"aliongea kijana aliyekuwa analima nyuma ya saluat kwa uchungu. Maneno Yale yalimchanganya sana saluat, alitamani aondoke hata kesho hapo kisiwani,ila ni jambo lisilo wezekana kabisa.
Masaa matatu yalipita tangu saluat afike shambani, amri ilitolewa kuwa kazi imeisha.wenyeji waliondoka wakiwa hoi hawana hata nguvu.
"WENYEJI" mkuu wa msafara alitoa amri,wote Wakasimama kusubiria yafuatayo.
"Tunahitaji wenyeji WATANO KWENDA KATIKA SHAMBA LA MHANDENI" alipomaliza kuongea mikono ya salu na Victor ilikuwa ishanyooshwa juu angani. Wengine walibaki wakiwashangaa ili wabidi kwani ilikuwa ni kama walilifahamu shamba hilo la mhandeni au vinginevyo hata baadhi ya wazawa wakiwashangaa walionyoosha mikono licha hawakuwaona kwa sura.
"NIMESEMA WATANO..WAWILI TANGULIANE MBELE" salu na Victor walianza kutoka wengine walifuata nyuma walipofika mbele walikuwa wametimia watano. Wengine waliondoka wakabaki wao pamoja na wazawa watano.
"KUANZIA KESHO MTAKUWA MNAENDA KWENYE SHAMBA LA MHANDENI HAWA WAZAWA WATAKUWA NANYI MNAWEZA KWENDA" Mkuu aliwaeleza, alipomaliza Waliondoka kuelekea sehemu ya Kulala.
Walipofika kwenye vyumba vyao walifanya usafi, walipomaliza walienda kula Kama kawaida saluat alikaa Meza moja na Victor wakipiga stori mbili tatu.
"MWENYEJI SALUAT" ilikuwa sauti ya mzawa wa kike ikiita. saluat alishtuka aliposikia jina lake linaitwa ila hakuitika aliamini Akina saluat watakuwa wengi sana. Victor alimuangalia saluat bila kusema chochote.
"MWENYEJI SALUAT HAYUPO" aliuliza raundi hii kwa ukali zaidi.
"salu wewe ndo unaitwa maanke hakuna salu mwingine" Victor alimwambia salu baada yakuona hakuna mwenyeji pale mwenye Jina kama Lake aliinuka nakuelekea alipo mzawa yule.
"KUMBE UPO ULIKUWA UNAJIVUTA NINI" alimuuliza kwa ukali.
"nilijua Kuna Saluat mwingine mzawa" alijitetea kwa uwoga sana.
"NIFUATE"alitoa amri Salu alimfuata mzawa yule, aliona wanatoka nje ya jengo lao muda si mrefu walifika kwenye Jengo lingine zuri sana waliingia ndani.
"UMEONA KILE CHUMBA (ALIMUONYESHEA)" Salu alitingisha kichwa kuashiria ameelewa vizuri.
"Utaenda pale ukifika fungua mlango" alimaliza nakuondoka, hakumwambia anaenda kukutana na nini au kufanya nini alibaki njia panda. Alijipa moyo nakuanza kutembea kukufikia chumba hicho, alipofika alifungua mlango mara pap!! Akakutana na mzawa Luka,alikuwa kama anamsubiria saluat. Saluat aliurudishia mlango WA chumba hicho.
"kwanini umeamua kwenda Handeni" aliuliza mzawa Lucas swali ambalo lilimshtua hata saluat. Kwani hakuelewa anamuuliza kama nani.
"ndyo nataka niende Handeni" alisisitiza
"HANDENI KUNA KIFO!! HIVI UNAKIELEWA UNACHOKIONGEA!!" alibadilika alikuwa kama anaongea na mtu ampendaye, ngurumo ya sauti yake ilijaa uchungu mwingi na macho yake yalikuwa na kila dalili yakulengwa na machozi, Salu alikuwa ametoa macho akimshangaa mzawa huyo aliyemfananisha na malaika hakuelewa amekumbwa na nini ila kama wasemavyo ujana nikuona mengi taratibu alishaanza kuelewa.
"Mzawa bado nataka kwenda kwenye shamba hilo" aliongea kwa kulazimisha ukakamavu huku akimuangalia mzawa huyo ambaye hakuwa mzawa tena bali Leo hii alikuwa Lucas mtupu kiasi chakumshtua saluat.
"KUNA MATESO KULE HAKUNA ANAYEPONA SALU WANGU" alisisitiza, mara hii alikuwa Salu wake, Salu alikuwa anaona mapichapicha tu.
"MZAWA LU-"
"SALU SITAKI KUKUPOTEZA" alikuwa amepiga magoti huku akiishikilia mikono ya salu........ ITAENDELEA...









Powered by Blogger.