-->

Header Ads

SPORTPESA WACHAFUA HALI YA HEWA, KUSITISHA UDHAMINI KWA KLABU HIZI..


SportPesa, kampuni ambayo inahusika na michezo ya bahati nasibu kwa nchi wa ukanda wa Afrika mashariki wametoa tamko la kuacha kudhamini timu zote za ligii kuu Kenya.

Kampuni hiyo imetangaza kujiondoa katika udhamini wa vilabu 10 ifikapo januari mosi 2018 kutokana na bodi ya mapato nchini Kenya kuongeza kodi katika michezo hiyo ya bahati nasibu kutoka asilimia 18 hadi 30.

Kiwango hicho cha kodi ambacho kitapunguza mapato katika kampuni za michezo ya kubahatisha kimewafanya SportPesa kupunguza gharama za matumizi ikiwemo udhamini wa vilabu nchini humo.
Haijuilikana kama tangazo hili litavihusu vilabu vya Tanzania vyenye udhamini na kampuni hiyo, Simba , Yanga na Singida United ingawa kwa Tanzania hakuna ongozeko lolote la kodi ambapo wanatozwa asilimia 18.
Powered by Blogger.