RAY AWAOMBA WATANZANIA WAMKUMBUKE KWENYE KIKI YAKE YA KUNYWA MAJI MENGI..
Msanii wa Filamu Bongo, Ray Kigosi baada ya kimya kirefu na kukosa habari mjini, anmeamua kuwakumbusha wabongo angalau kumtania kwa ishu yake ya kunywa maji mengi ili aendelee kuwa kwenye gemu la bongo movie naa kupata ishu za ubalozi kama ule wa maji ya AFYA. Hii niu kuhusu kuwa weupe wake unatokana na kunywa maji mengi na kufanya mazoezi na si kujichubua kama wengi wanavyodhani.
Kupitia mtandao wa instagram Ray amekuja na hii mpya, ameandika maneno haya haya na kuweka hiyo picha hapo juu. “Kuna wakati mwingine ukikaa kimya unaweza ukaufanya uongo ukawa ukweli.. swali langu ni moja kwenu nyie mnaosema najichubua hivi ni kweli mnamjua mtu anayejichubua?,” amehoji Ray na kuendelea.
“Embu niangalieni vizuri mtapata jibu, tatizo letu sisi Watanzania tunapenda sana kuaminini uongo kuliko ukweli. Nilishawaambia ukitaka kuwa na ngozi yenye nuru kama yangu fanya sana mazoezi kunywa sana maji, hiyo ndio dawa mbona hata madoctor wanalijua ilo,” amemaliza kwa kuandika.
Kama kawaida ya wabongo kwenye comment wakatiririka vizuri tu......
No comments