-->

Header Ads

MRISHO NGASSA: Sina matumaini na YANGA SANA MAANA MANENO YAMEKUWA MENGI

Nyota huyo wa zamani wa klabu za Yanga, Simba na Azam amesema alikuwa na mpango wa kurejea Yanga, lakini uongozi wa timu hiyo umekuwa kimya

Kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Mrisho Ngassa amesema bado yupo kwenye harakati za kutafuta timu ya kucheza msimu ujao baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita na timu hiyo ya Mbeya.

Ngassa amesema, mipango hiyo inafanywa na wakala wake ambaye ni Baba yake Khalfani Ngassa na itakapokuwa tayari atamweleza ni wapi pakwenda.

“Bado sijajua ni timu gani nitacheza msimu ujao iwe ni hapa nyumbani au nje ya Tanzania lakini bado jitihada zinafanyika kuona ni sehemu gani naweza kufanya kazi msimu ujao,” amesema Ngassa.

Nyota huyo wa zamani wa klabu za Yanga, Simba na Azam amesema alikuwa na mpango wa kurejea Yanga, lakini uongozi wa timu hiyo umekuwa kimya kwa muda mrefu hivyo bado anasikilizia nini kitakachotokea baadaye.

Amesema awali alikaribia kusaini lakini viongozi waliopo walipata maelekezo kutoka kwa kocha wao George Lwandamina kuwa asubiriwe yeye hivyo ndiyo anasubiri.

“Bado nasubiri mpango wa Yanga, lakini sina matumaini sana maana maneno yamekuwa mengi chamsingi namsikilizia meneja wangu ni wapi atanipeleka kufanya kazi msimu ujao,” amesema.

Ngassa ambaye pia aliwahi kutamba na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars amesema, kama mipango yake ya kwenda nje au kujiunga na Yanga kushindikana yupo tayari kubaki Mbeya City endapo timu hiyo itampa dau nono atakalo hitaji.

No comments

Powered by Blogger.