-->

Header Ads

Shule zilizoshika mkia matokeo ya kidato cha sita walimu wao wazungumza




Wakizungumzia matokeo mabaya ya shule zao, baadhi ya walimu walisema matayarisho duni, kupokea wanafunzi waliofanya vibaya kidato cha nne, ndiko kulikowaponza.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Hagafilo mkoani Njombe, Castory Kayombo alisema walitarajia matokeo hayo kutokana na aina ya wanafunzi waliokuwa wamewapokea.

“Tulipokea wanafunzi ambao walikuwa hawajiwezi darasani, wengi walikuwa na daraja la nne kwenye matokeo ya kidato cha nne, hivyo licha ya kujitahidi kuwafundisha, ndio tumeambulia matokeo hayo,” alisema.

Hata hivyo, alisema wataendelea na mikakati yao ya kufanya vizuri ili mwakani, wasipate matokeo ya mwisho kama ilivyo mwaka huu.

Mmoja wa walimu wa Shule ya Sekondari Meta, jijini Mbeya Neema Matonya alisema bado hawajapata matokeo hayo na kwamba, kwa sasa hawawezi kuzungumza lolote.

“Bado hatujayapata hayo matokeo kwa hiyo hatuwezi kuzungumza lolote,”alisema

Kama unamaoni ama ushauri kuhusiana na matokeo ya kidato cha sita na unataka kushare tutumie kupitia    >>>Hapa<<< au kupitia no. 0719600096 nasi tutayapost.

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.