-->

Header Ads

WAYNE ROONEY BADO HAKIJAELEKA MSIMU UJAO, NJIAPANDA UNITED



Mambo hayaeleweki kwa Wayne Rooney pale Old Trafford kwani hana uhakika na namba kwenye kikosi cha Jose Mourinho

Manchester United wanaonekana hawapo tayari kumuuza Wayne Rooney kwa bei rahisi.

Inaaminika kuwa United wapo tayari kuachana na nahodha wao baada ya kucheza mechi chache sana msimu uliopita Jose Mourinho akiwa kocha Old Trafford.

Amehusishwa na tetesi za kutaka kujiunga na Everton au China lakini kwa mujibu wa Mirror, bado hajapokea ofa nzuri.

Everton wanaonekana kutokuwa tayari kukidhi mahitaji ya Wayen Rooney, wakati mpango wa kwenda China ukionekana kuwa mgumu sasa baada ya kuanzishwa kwa utaratibu mpya wa kodi kwa wachezaji wa kigeni.

United hawapo tayari kumuuza Rooney kwa dau la chini ya thamani yake au kuchangia mshahara wake kwa klabu nyingine, kwa hiyo pande zote zinabaki njia panda.

Kipindi cha kampeni zilizopita Ligi Kuu Uingereza, Rooney mwenye umri wa miaka 31 alianza mechi 25 kwenye kikosi cha United kilichoshinda Kombe la EFL na Europa.

No comments

Powered by Blogger.