-->

Header Ads

BREAKING: SAKATA LA JOHN MNYIKA KUTOLEWA BUNGENI, WABUNGE WA UPINZANI WAJA JUU!!..

Image result for JOHN MNYIKA BUNGENI




Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ametolewa nje ya Bunge leo Ijumaa kwa agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Licha ya adhabu hiyo, amemzuia kutohudhuria vikao vya Bunge kwa siku saba kuanzia leo.

Mnyika ametolewa baada ya mmoja wa wabunge kusema 'Mnyika mwizi' akimhusisha na wizi wa madini, hoja inayochangiwa na wengi kwenye mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini unaoendelea.


Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua kwa mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika akasema hajui hilo na haijaingia kwenye hansadi. Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayaweze kwenda hivyo.

Baada ya majibizano kati yake na Spika, Spika akaamuru walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge na asihudhurie vikao saba vinavyofuata.

Mnyika alikuwa akitoa maelezo baada ya Mbunge wa Mtera, Livingston Lusinde kusema upinzani wa Tanzania ni wa ajabu kwani unatetea wezi wa madini.

Kufuatilia tukio hilo Wabunge wa Upinzani wametoka nje baada ya Mbunge huyo kutolewa nje na Askari wa Bunge kwa amri ya Spika.

Vilevile, Mamlaka ya Bunge kupitia Kamati ya Maadili kumjadili Mbunge Esther Bulaya kwa kuhamasisha wabunge kutoka nje ukumbi wa Bunge

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.