-->

Header Ads

MBUNGE GODBLES LEMA ALIA KUTENGWA KUTOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI JIMBONI KWAKE MBELE YA MAKAMU WA RAIS MSIBANI


Mbunge wa Arusha mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo mheshimiwa Godbless Lema amesikitika kitendo cha kunyimwa nafasi ya kutoa salamu za rambi rambi kwenye shughuli ya kuaga miili ya wanafunzi,walimu pamoja na dereva wa shule ya msingi Lucky Vicent waliofariki kufuatia ajali ya basi mapema asubuhi juzi.Katika ukurasa wake wa facebook mbunge huyo ameandika hivi

Leo katika msiba wa kuaga Wanafunzi waliofariki katokk ajali, Mimi kama Mbunge mwenyeji niliyefiwa Jimboni kwangu pamoja na Mayor tulihudhuria maombolezo hayo, ilikuwa ni itifaki ya kawaida kabisa kuelewa kuwa Mbunge pamoja na Mayor watapaswa kutoa salamu za rambi rambi au kuwashukuru wageni waliofika kwa ajili ya kutupa pole .

Nilisikia toka jana jioni kuwa katika maombolezo haya leo kuwa Viongozi wa Chadema watapaswa kutokuongea , nilimpigia simu Mbunge wa Ngorongoro Mh Ole Nasha , nikamweleza ubaguzi mchafu unavyopangwa katika jambo hili muhimu la kuaga watoto wetu, alinihakikishia kuwa Makamu wa Rais asingeweza kukubaliana na ujinga huu.

Kwenye ratiba nilipoingia uwanjani , jina langu lilikuwepo kwenye ratiba kwa ajili ya salamu za rambi rambi , lakini baada ya Mkuu wa Mkoa kukabidhiwa itifaki , mambo yalibadilika na ilionekana dhairi kuwa sitakiwi kabosa kutoa pole kwa watu wa jimbo langu waliofikwa na msiba huu mbaya. Mkiti Mbowe aliandika meseji kwenda kwa M/ Rais kukumbusha umuhimu wa wenyeji kutoa salamu , Makamu wa Rais baada ya kupokea meseji hiyo , alimwita Mkuu wa Mkoa , ndipo ilionekana kama kuna ushindani unatokea kati yao , lakini hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kutoa salamu kwa wapendwa wetu.

Wabunge wa ccm waliokuwepo ambao ni mawaziri wote waliweza kutoa pole ,huu ni ubaguzi uliojaa ujinga na chuki mbaya kisiasa , nitaueleza madhara yame kwenye hotuba yangu kesho , lakini nafikiri watoto wanafuata walichofundishwa na wazazi ,pengine ingekuwa ni usaliti Mbunge Lema kusalimia na kuwapa pole watu wake mbele ya Makamu wa Rais . Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama Nchi na Syria ni wakati.

Nawashukuru wote waliotukimbilia kwa matatizo yaliyotokea Arusha , Mungu awabariki sana. Msiogope , Mungu hadhiakiwi apandacho Mtu ndicho avunacho




JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.