-->

Header Ads

TSNP: TUTAWAFIKISHA MAHAKAMANI WAANDAAJI WA MISS TZ


Kurugenzi ya sheria ya TSNP (Tanzania Students Networking Program/Mtandao wa Wanafunzi Tanzania), imepokea malalamiko kutoka kwa walimbwende  walioshiriki kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2016 na kushika nafasi ya 2,3 na 4, kutolipwa fedha zao  walizoahidiwa na waandaaji wa mashindano hayo (Lino International Agency Ltd).

Walimbwende hao ni Mary Peter Clavery (Miss Tz # 02), Grace Christopher Malikita (Miss Tz # 03) na Anna Nitwa (Miss Tz # 04). 
Tayari mawakili wetu wemepitia mikataba yao na kujiridhisha pasna shaka kuwa imekiukwa na waandaaji hao.

Mawakili wetu wako mbioni kuwasilisha kwa kampuni hiyo muda wowote kuanzia sasa, notisi ya madai na kusudio la kuwafikisha mahakamani ikiwa watashindwa kuwalipa walimbwende hao fedha zote wanazowadai kwa muda watakaolekezwa (demand notice and intention to commence legal proceedings).

TSNP tumekubali kubeba suala hili kwani walalamikaji ni wanafunzi na kwa mujibu wa majukumu ya kikatiba ya taasisi yetu ni pamoja na kulinda, kutetea na  kupigania haki za wanafunzi wote wa Tanzania. 
Pia, tunaamini kuwa, kwa kudhibiti hali hii inayoweza kutafsiriwa kama utapeli, ubabaishaji au vyovyote vile inavyoweza kutafsiriwa, tutakuwa tumejenga msingi sio tu wa kuondoa mambo hayo yanayotia aibu mashindano hayo na kukanyaga haki za washiriki, bali tutakuwa tumetoa funzo kwa waandaaji hao kutorudia aina hii ya mashindano.

Tutawafahamisha zaidi katika kila hatua ya kushughulikia jambo hili.
_______________
©Bob Wangwe
Mkurugenzi wa sheria TSNP

No comments

Powered by Blogger.