KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI NA MADHARA YAKE
KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI NA MADHARA YAKE
Kujifungua kwa njia ya upasuaji au Cesarean section delivery ni njia ya kujifungua mtoto kwa upasuaji kupitia tumbo la mama.
Mchano wa kwanza hufanyika kwenye tumbo na wa pili kwenye kizazi ambapo mtoto hutolewa. Mara nyingi kujifungua kwa njia hii hupangwa pale ambapo umepata shida wakati wa ujauzito inayohitaji kujifungua kwa upasuaji au wale waliojifungua kwa upasuaji mara ya mwisho.
Kujifungua kwa njia ya upasuaji kunaweza kuwa salama kwako na kwa afya ya mtoto pale;Uchungu wako hauendelei vizuri
Hii ni baada ya mjamzito kuingia kwenye uchungu na mtoto kutoshuka vizuri, kutokana na mtoto kuwa mkubwa au shingo ya uzazi kutofunguka.
Mtoto hapati hewa ya kutosha
Mapigo ya moyo ya mtoto yakiongezeka sana wakati wa uchungu huashiria mtoto hapati hewa ya kutosha, na hivyo kuwahishwa kwa ajili ya upasuaji.
Mtoto amelala vibaya tumboni
Upasuaji unaweza kutumika kama mtoto amelala vibaya tumboni mwa mjamzito, au wakati akiwa ametanguliza matako au miguu.
Ujauzito wa mapacha au zaidi
Wakati mwingine ujauzito wa mapacha au zaidi unaweza ukajifungua kwa njia ya upasuaji.
Kondo la uzazi kujiachia mapema
Hali hii huitwa abruptio placenta , ambapo kondo la uzazi hujiachia mapema kabla ya uchungu kuanza. Huhatarisha afya ya mama na mtoto, hivyo mjazito hufanyiwa upasuaji wa dharura ili kujifungua.
Kama uliwahi kujifungua kwa upasuaji
Kama ulijifungua kwa upasuaji mara ya mwisho, unaweza kuendelea kujifungua kwa njia hiyo endapo kujifungua kwa kawaida kutaleta hatari.
Hatari za Kujifungua kwa njia hii:
Kwa mtoto Matatizo ya kupumua
Mtoto kuumizwa, ingawa ni mara chache sana kutokea
Kwa Mama
Maambukizi ya tumbo la uzazi ( endometritis )
Kupoteza damu nyingi
Damu kuganda kwenye mishipa ya kiuno au miguu
Kidonda kupata maambukizi, kuchelewa kupona au kufumuka
Wakati mwingine kibofu cha mkojo kinaweza kuumizwa wakati upasuaji unafanyika.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments