-->

Header Ads

MANENO YA ZITTO KABWE BAADA YA WAKILI Alberto Msando KUJIUZULU


Wakili Alberto Msando amejiuzulu nafasi yake ya ushauri wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne na kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe imeeleza kuwa Msando ameandika barua ya kujivua wadhifa huo ambayo imepokelewa na chama hicho.

“Ndugu Msando anawajibika kwani anapaswa, nanukuu  ‘kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka.’Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama,”amesema Zitto.

Zitto amesema Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya ACT.

“Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake. Msando ameomba msamaha kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba,”amesema Zitto.






JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.