-->

Header Ads

MAZUNGUMZO YA SIMU KATI YA RAIS WA UFARANSA NA IRAN YAZUA GUMZO



Emmanuel Macron, Rais mpya wa Ufaransa amesisitiza juu ya kudumishwa na kuimarishwa uhusiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Macron amesema hayo katika mazungumzo yake ya simu na Rais Hassan Rouhan ambaye alishinda katika uchaguzi uliofanyika Ijuaa iliyopita hapa nchini.

Katika mazungumzo hayo, Rais wa Ufaransa sambamba na kumpongeza Rais Rouhani kwa kuchaguliwa tena katika uchaguzi alioutaja kuwa muhimu na uliohudhuriwa na wengi amesisitiza juu ya azma ya Paris ya kustawisha ushirikiano wake na Tehran katika nyanja mbalimbali.  Nchi ya Ufaransa ilikuwa na nafasi muhimu katika kufikia natija mazungumzo ya Iran na kundi la 5+1. Hata kama katika utekelezwaji wa makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) kumekuweko na changamoto, lakini pamoja na hayo, safari ya Rais Rouhani miaka miwili iliyopita huko Paris Ufaransa, ilionyesha umuhimu wa uhusiano kati ya Iran na Ufaransa. Ni kwa kuzingatia ukweli huo, ndio maana katika mazungumzo yao ya kwanza Marais wa Ufaransa na Iran wametilia mkazo jambo hilo.

Makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ni miongoni mwa mambo ambayo yanakabiliwa na ugumu katika utekelezaji wake kutokana na ukiukaji ahadi wa Marekani. Kuweko vizingiti vya miamala ya kibenki na kifedha katika njia ya ustawishaji uhusiano wa kiuchumi na kibiashara wa Iran na nchi za Ulaya ikiwemo Ufaransa, vinahesabiwa kuwa moja ya changamoto kubwa katika njia hiyo.

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.