-->

Header Ads

PLUIJM KUVUNA WACHEZAJI YANGA. SINGIDA UNITED YA MOTO.

Oscar Joshua na Ally Mushapha "Bartez" ni wachezi ambao wamekosa nafasi ya kucheza chini ya kocha Lwandamina na kufanya nafasi zao kubaki msimu ujao kuwa ndogo.

Taarifa kutoka kwa kiongozi ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema kuwa wachezaji hao watatolewa kwa mkopo kwenda Singina United kuungana na kocha wa Yanga wa zamani, Hans Van Pluijm.

Wachezaji hao ambao wamebakiza mwaka mmoja kabla mikataba yao kuisha Yanga, wamepata ofa hiyo kutokana na Pluijm kuhitaji huduma zao.

Baada ya kutafutwa Bartez kuthibitisha taarifa hizi alisema kuwa hana taarifa rasmi hivyo kwa sasa yeye ni mchezaji wa Yanga na anasubili taarifa kutoka kwa uongozi kujua hatima yake.

Usajili huo ukikamilika Singida United itakuwa ya moto kutokana na kufanya usajili wa maana na wa gharama. nafasi pekee ambayo bado haijafanyiwa usajili ni ya golikipa ambao Bartezi na Aishi Manula wa Azam wakihusishwa kuchukua nafasi hizo.

No comments

Powered by Blogger.