RASMI; MSUVA RUKSA KUONDOKA YANGA, MWENYEWE AWEKA NGUMU.. SABABU HII
Baada ya wakala wa Saimon Msuva, Jonas Tibahola kulalamika kwa vyombo vya habari kuwa klabu ya Yanga wanaweka ngumu kumuachia mchezaji wake akacheze soka la kulipwa.
Klabu ya Yanga kupitia kwa katibu mkuu wake, Mkwasa wametoa tamko rasmi kuwa Msuva yupo sokoni na wapo tayari kumuachia kuondoka endapo makubaliano yatafikiwa baina ya Klabu mbili husika.
Inasemekana Msuva amepata soko katika nchi za kiarabu ambapo klabu mbali mbali kutoka Misri, Tunisia na Morroco kuhitaji huduma ya mchezaji huyo.
Ofa ambayo inasikilizwa kwa sasa ni kutoka klabu moja inayoshiriki ligi kuu Morroco ambayo imeshika nafasi ya pili katika msimamo, Difaa El Jadid wapo tayari kutoa kiasi cha Tsh 177 milioni kama ada ya uhamisho na mshahara wa 9 milioni kwa Msuva.
Inasemekana Msuva amegomea mshahara huo akidai nyongeza huku pia klabu ya Yanga wakidai 300 milioni kama thamani ya ada wa uhamisho wa mchezaji hiyo. bado mazungumzo yanaendelea vizuri baina ya pande mbili kufanikisha dili hilo.

No comments