-->

Header Ads

TAHARUKI!! ZAWADI NONO YATANGAZWA KWA ATAEPELEKA KICHWA CHA WAZIRI MKUU

Msomaji wa AKISITV ukitangaziwa kulipwa dau kubwa kupeleka kichwa cha kiongozi wako utafanya hivyo!

Wengine ndio wengine hapana lakini kule nchini India wananchi wamejawa na gadhabu baada ya tangazo lililotolewa la malipo ya rupia milioni moja kwa ateweza kupeleka kichwa cha waziri mkuu Mamata Banerjee.

Tangazo hilo limetolewa na mshiriki wa chama tawala nchini humo BJP ambapo ameahidi kutoa rupia milioni 1.1 ($17,018; £13,622) kwa yule atakayemletea kichwa cha waziri mkuu wa jimbo la magharibi mwa Bengal Mamata Banerjee.

Hata hivyo chama cha BJP kilikana tangazo hilo.
Bi Banerjee ni mwanasiasa maarufu aliyetajwa kati ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani katika nakala ya Times mwaka wa 2012.

Bwana Varshney ni mshiriki wa mrengo wa vijana katika chama tawala cha Bharatiya Janata

Ripoti zilisema kuwa polisi walikataa kuwapa ruhusa ya mkutano huo kufanyika siku ya Jumapili katika jiji la Birbhum, kilomita 180 kutoka kwa mji mkuu Kolkata ( iliyokuwa Calcutta) na kuivunja mkutano huo kwa kutumia nguvu ilipojaribu kuingia eneo hilo linaloongozwa na waislamu.

Chama cha Bi Banerjee cha All India Trinamool Congress limeikashifu vikali tangazo hilo na kudai kushikwa kwa bwana Varshney.
Wahindi wengi pia walienda kwa mitandao ya kijamii kukashifu vitisho hivyo.

No comments

Powered by Blogger.