-->

Header Ads

RASMI: Wajumbe wa kamati ya pili kuchunguza mchanga wa madini waapishwa



Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Longinus Kyaruzi Rutasitara kuwa mjube wa  Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017


Walioapishwa leo Ikulu, jijini hapa ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa Nehemiah Eliachim Osoro na wajumbe wake ambao ni Profesa Longinus Kyaruzi Rutasitara, Dk Oswald Joseph Mashindano.

Dar es Salaam. Rais John Pombe Magufuli, amewaapisha wajumbe wa Kamati Maalum ya pili ya wachumi na wanasheria itakayochunguza mchanga wenye madini ulio katika makontena yaliyopo maeneo mbalimbali nchini.

Walioapishwa leo Ikulu, jijini hapa ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa Nehemiah Eliachim Osoro na wajumbe wake ambao ni Profesa Longinus Kyaruzi Rutasitara, Dk Oswald Joseph Mashindano.

Wengine ni Casmir Sumba Kyuki, Andrew Wilson Massawe, Gabriel Pascal Malata, Usaje Bernard Usubisye na Butamo Kasuka Philip.

Akizungumza baada ya kuwaapisha wajumbe wa kamati hii, Rais Magufuli amesema ameunda kamati hiyo ili ifanye uchunguzi wa kina utakaobaini aina ya madini yaliyo ndani ya mchanga huo, thamani yake, kiwango cha kila aina ya madini, uzito wa mchanga unaowekwa ndani ya makontena na pia kujua ni makontena mangapi yamepitishwa tangu mwaka 1998.

“Kafuatilieni makontena mangapi yametoka hapa nchini na kupelekwa nje ya nchi tangu mwaka 1998, na kama hayo makontena yana madini aina ya dhahabu, shaba na silva mkafuatilie tujue zimepelekwa tani ngapi za dhahabu, tani ngapi za shaba na tani ngapi za silva, je makontena mangapi yanapita kila mwezi? Makontena 1,000 au mangapi? na je zilikuwa na thamani ya kiasi gani? Je tumelipwa kiasi gani cha fedha?


MWANANCHI.



JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.