-->

Header Ads

Mitazamo tofauti kuhusu Wimbo wa daimond


Mama ananiambia NASEEB, Mimi ni Mtu mzima na wewe ndio nakugemea.
Yanayotokea Jaribu, kupiga Kimya usidiliki hata Kuongea.
Mara nasikia vya Aibu, MAKONDA kwa GWAJINA eti Ugomvi umekolea.
Kuchunguza karibu, Ni Binti Mmoja kwa Mitandao anachocheaa...
Najaribuu kunyamaza, ila Moyo hautaki. Unanambia eti SIMBA japo Nguruma uiseme haki.
Ooh! Najaribuu kunyamaza, hata XTEEZY hataki Yoyooh!, Anasema walau nena kidogoo...
Hiih!!
Na Mashabiki DANGOTE,
Wananiambia mbona husemi Chochote,
Aah! siuko nao siku zote,
Ama Ulezi unafanya Uogope,
Aah! na Media Pande zote,
Wanalalama Kiongozi atoke,
Eeh! Nchi inaingia Matope,
Niende wapi na Mimi Mtoto wa wote,
Yaani Lawamaa...
[CHORUS]
Acha Nikae Kimya(Nisiongee)
Nikae Kimya(Oh Ninyamaze Mimi)
Kinya(Nisiseme)
(VERSE 2)
Mmh! Ni Mengi Najaribu, najitahidi Epuka yasije nicost, Japo mengine Swadakta, Mengine hayana maana..
Rafiki kipenzi wa karibu, hata Nyimbo yake sikuweza ipost, Ila alipokamatwa iliniumiza sanaaa......
#ACHA_NIKAE_KIMYA ya Diamond Platinum
Ni katika wimbo wake mpya uitwao bora nikae kimya. Diamond amegusia ugomvi wa Makonda na Gwajima na ushiriki wa Mange. Amegusia tatizo la vyeti la Makonda na shinikizo la kutaka atenguliwe.
Katika wimbo huo mpya amegusia wimbo wa Ney na kukamatwa kwa Ney, kupotea kwa Roma.
Ametumia fasihi ya hali ya juu lakini wimbo huu unamuweka kwenye kundi la waoga wanaohofia maisha yao. Diamond anasema kwenye wimbo huo ameonywa na mama yake juu ya kusema chochote kwa yanayotokea.
Anasema kumekuwa na shinikizo kutoka kwa mashabiki wakimtaka aseme chochote kuhusiana na yanayoendelea na wengine wakimtuhumu kuwa anaogopa kusema kwa kuwa Makonda ni mlezi wa Wasafi.
Diamond anasema alishindwa kupost wimbo wa nay japo ni rafiki yake wa karibu (kwa sababu ya maudhui) lakini aliumia sana Nay alipokamatwa.
Amegusia pia mgogoro ya CCM na CHADEMA.
Ametumia ufundi wa kisanaa hasa kuwasilisha ujumbe wake, lakini wimbo huu unaweza kutafsiriwa kuwa anaonyesha woga katika kuipigania jamii yake na kukemea maovu katika jamii.
Pia udhaifu mwingine ni kwamba kutumia neno "eti" kwenye swala la kuvamiwa kwa clouds media kunamuweka upande wa wavamizi kwani anatilia shaka swala ambalo ni dhahiri lilitokea
Zawadi B Lupelo/JF
Visit website
Mange kimambi anasemaje..
Mange Kimambi hajapendezwa na Wimbo mpya wa Diamond "Acha nikae Kimya" Amemshukia Diamond Kama Ifuatavyo:
"We Pu... unatumika vibayaaaaaa.Hiyo kitu ya kuwatishia watanzania na vita sijui ukosefu wa amani CCM washaitumia for many years kuwatisha watanzania.Watu wakitaka mabadiliko gia Yao ya kwanza ni kuwatishia kuwa amani itapotea. Acha ipoteeee, Amani ya kisenge ya nyinyi wachache kutajirika kujenga mastate house sijui ushenzi gani Huku wengine wanasaga meno tumeichoka.wewe Dai umeshashiba huoni shida ya wengine lazma utake Amani, kamuulize anaeshinda mlo mmoja kama kuna Amani Tz?
You call this Amani? Amani ya vyama vya siasa kunyimwa kufanya mikutano ya hadhara, Amani ya Wa Bunge wa upinzani kufungwa jela kila siku? Amani ya vyombo vya habari kuvamiwa kwa mitutu? Amani ya wananchi kutajwa kama wauza unga ili waibiwe mali zao? Amani ya watz kutishiwa kuuwawa sababu ya kuandamana kitu ambacho kinaruhusiwa kikatiba?Amani ya wasaniii kutekwa sababu kiongozi anatafuta Kiki za ki....., Hiyo Amani ya ki... hatuitaki. Dai Ungemsikilzia mamako na unyamazeeee.Ndio sisi watz tulio nje ya Tz ndo tunaongea sana , hilo tu ni ushahidi tosha kuwa Tz hakuna Amani kwanini walioko ndani waogope kusema tuseme sisi tulioko nje?
Dai embu tuliza P... hizo! Kama umekosa cha kufanya kamtie .... mfanye arobaini maana ndo kiki ulizobakiza siku hizi.Kwenye issue za msingi usilete P... zako. F.... wewe!" Mange Kimambi
TOA MAONI YAKO!

No comments

Powered by Blogger.