Lulu Kortini Tena Leo Kesi ya Kifo cha Kanumba – Vide
Jana mahakamani hapo, Mdogo wa Kanumba, Seth alitoa ushahidi wake akiieleza mahakama kwamba anachofahamu yeye ni kuwa palikuwa na mgogoro kati ya Lulu na Kanumba aliousikia ambapo Lulu alikuwa akiongea kwa simu na mwanaume mwingine hali iliyozua ugomvi huo na Kanumba.
Leo mashahidi watatu wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kwenye kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.