Torres: 'Morata ni miongoni mwa mastraika bora'
Morata, 24, amekuwa na mwanzo mzuri kwenye kikosi cha Blues baada ya kusaijiliwa kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 60 akitokea Real Madrid, amefunga magoli sita katika mechi sita za Ligi Kuu Uingereza, ikiwa ni pamoja na hat-trick dhidi ya Stoke City wikiendi iliyopita.
Torres anaikaribisha timu yake ya zamani kwenye uwanja wa Wanda Metropolitano katika mechi ya Ligi ya Mabingwa na hilo ni jaribio gumu kwao kwani wanakwenda kukabiliana na Morata miongoni mwa wachezaji hatari Chelsea.
"Nilizungumza naye kabla hajajiunga na Chelsea na nilimwambia nitakuwa nikipatikana kwenye simu ikiwa atahitaji ushauri wowote au msaada ninaoweza kumsaidia," Torres aliliambia The Mirror. "Nikiangalia jinsi alivyoanza msimu, sidhani kama anahitaji ushauri wowote - tayari anacheza vizuri na anafunga magoli mengi.
"Chelsea mepata mastraika bora Ulaya - na nina uhakika anakwenda kushinda mataji pamoja na timu hiyo.
"Mechi ya Chelsea haitakuwa rahisi - kuna sababu ya wao kuwa mabingwa Uingereza. Ni miongoni mwa timu ambazo naamini zinaweza kutwaa ubingwa Ulaya msimu huu.
"Timu zote Ulaya zimekuwa thabiti sana mwaka huu - zote zimesheheni wachezaji wenye ubora wa hali ya juu na wote wanajiamini."
Atletico itachuana dhidi ya Chelsea leo baada ya kulazimishwa sare na Roma katika mechi ya kwanza wakati Chelsea ikiwa kileleni mwa kundi C baada ya kuigaragaza Qarabag 6-0.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments