Jinsi ya kutibu vidonda vya kooni
Uvimbe kooni husababishwa na mambo mengi na mara nyingi huwa haisababishi shida kubwa sana.Ukifungana mapua, makamasi hupitia kooni na hivyo basi kusababisha uvimbe.Baridi kavu inaweza pia kufanya koo likauke na mtu ahisi likiwashawasha.Unaposhikwa na mafua, pia unaweza kusababisha kidonda kooni kinachoweza tu kutibiwa na dawa.
Jinsi ya kutibu vidonda vya kooni:
- Sukutua maji ya chumvi yaliyo vuguvugu
- Mumunya dawa za koo, usiwape watoto inaweza kumnyonga akimeza kwa bahati mbaya.
- Muulize mfamasia wako akuuzie kipulizo (spray) cha kutuliza uchungu kooni.
- Ikiwa koo linawasha au limekauka, pumua mvuke wa maji moto itakusaidia.
Muite daktari ikiwa:
- Umefura tezi za limfu shingoni.
- Una mabakabaka meupe huko nyuma ya koo lako.
- Kwa gafla tu unashikwa na kuumwa na koo huku ukiwa na joto jingi.
- Koo linavimba na kuuma zaidi ya juma moja.
- Ukishindwa kunywa chochote umu hatarini mwa kuishiwa maji mwilini.
- Huku mbele kwa shingo lako pia kumevimba pamoja na koo lako
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments