PICHA: HIVI NDIVYO SAMATTA ALIVYOIONGOZA STARS KUIANGAMIZA BOTSWANA
Mabao mawili ya nahodha Mbwana Samatta anayeichezea klabu ya KRC Genk, yametosha kuipa Tanzania, ‘Taifa Stars’ ushindi wa mabao 2-0, Botswana huo ukiwa ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Ushindi huo umemkaribisha vizuri kocha Salum Mayanga na Waziri mpya wa michezo Harson Mwakyembe ambae naye alihudhuria kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa kuchukua nafasi ya Nape Nnauye jana.
Ushindi huo umewafuta majonzi Watanzania, ambao kwa muda mrefu hawajapata ushindi kwenye aridhi yao ya nyumbani.
Samtta aliwafungia wenyeji Taifa Stars, bao la mapema dakika ya pili na kuwavunja nguvu wapinzani wao Botswana wanaofundishwa na kocha Peter Butler.
Botswana walijitahidi kupambana kusawazisha bao hilo lakini walinzi wa Tanzania Erasto Nyoni na Abdi Banda walikuwa makini kuondosha hatari zote langoni mwao.
Botswana walifanya shambulizi kali dakika ya 26 lakini shuti la Omaatla Kessgle liligonga mwamba na mpira kurudi uwanjani kalba ya kuokolewa na mabeki wa Stars.
Winga Simo Msuva alipata nafasi ya wazi dakika ya 32 lakini shuti lake halikuweza kulenga lango nafasi kama hiyo aliipata Ibrahim Ajibu dakika ya 36 lakini mpira alioupiga ulipaa juu la lango la Botswana.
Kipa Kabelo Dambe, alifanya kazi ya ziada dakika ya 39 baada ya kupangua shuti la Msuva na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda kwa wenyeji Tanzania.
Mchezo huo uliendelea kwa Tanzania kuutawala mchezo na kushambulia huku Botswana wakifanya mashambulizi ya kustukiza na matokeo kubaki hivyo hadi mapumziko.
Kipindi cha pili Botswana walikuja juu na kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Taifa Stars na Ookeditse Semelemela.
Tanzani walirudi mchezoni na kuanza kuliandama lango la Botswana, lakini Msuva alipoteza nafasi ya wazi baada ya pasi nzuri ya Samatta dakika ya 54.
Farid Mussa aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Shiza Kichuya, alipoteza nafasi ya wazi baada ya kazi nzuri ya Samatta, lakini mabeki wa Botswana walimzonga na kuanguka chini.
Samatta alipata nafasi nzuri akiwa yeye na kipa wa Botswana lakini kipa huyo alifanya kazi nzuri kwa kupangua mpira huo na kuwa kana.
Dakika ya 87 Samatta alifunga bao la pili, baada kupiga mpira wa adhabu ndogo uliokwenda wavuni moja kwa moja na kumuacha kipa Kabelo Dambe akiruka bila mafanikio.
Bao hilo lilionyesha kupoteza matumaini ya Botswana ambao kipindi cha pili walicheza vizuri na kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la wenyeji wao.

No comments