"Ni lazima waniue" - Msigwa

Mbunge wa Iringa
Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema atalishitaki Jeshi la Polisi, kwa
tuhuma za kuingilia majukumu yake ya kikazi pale anapokuwa akitimiza
wajibu wake wa kibunge ikiwa pamoja na kuzungumza na wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
Jumatatu, Mchungaji Msigwa amesema chombo pekee kinachoweza kumtia
hatiani kwa kufanya uchochezi ni mahakama na sio polisi.
“Jana walinikamata tangu saa
11:30 na kuanza kunihoji mpaka saa 3:15 usiku kwa tuhuma za kufanya
uchochezi lakini mimi nakakataa sijafanya uchochezi kwa sababau hakuna
mtu anaweza kunizuia kuongea na wananchi wangu, wanadai nimeleta hofu
na kuvichonganisha vyombo vya dola na wananchi,” amesema Msigwa .
Mh. Msigwa ameongeza kwamba “Mimi
niko tayari hata kama wangeniweka ndani wiki mbili siogopi kwa sababu
sitanyamaza nitaendelea kuongea na sitaacha kusema kilichomtokea Tundu
Lissu na ili kuninyamazisha ni lazima waniue kwa sababu nimeshajiandaa
kisaikolojia,” amesema Mchungaji Msigwa.
Akizungumzia hilo Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Iringa, Julius Mjengi amesema walimkamata Msigwa kwa kuwa alikuwa
anatoa maneno ya uchochezi kwa wananchi aliokuwa anawahutubia mkutano wa
hadhara Kata ya Mlandege na kuongeza kuwa jeshi hilo linaendela na
upelelezi juu ya tuhuma hizo na mara utakapokamilika watamfikisha
mahakamani.
Aidha Mchungaji Peter Msigwa amesema mpaka muda huu yupo nje kwa dhamana.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments