Nikki awachana Janjaro na Young Dee
Nikki
wa Pili amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya
kupita siku kadhaa tokea Dogo Janja kutoa kauli yake ya kukataa
kufananishwa na Young Dee kwa madai ni 'mteja wa unga' jambo ambalo
lilizua makelele mengi kwa mashabiki wa wasanii hao pamoja na meneja
wake Young Dee.
"Mimi naona kuna tatizo
hapo, kwa sababu wameanza kuhusisha maisha yao binafsi, kwa hiyo
ningefurahi kuona wanashindana kimuziki zaidi. Maana unapokuwa maarufu
ukiongea kitu ujue kinaishi kwa kipindi kirefu na hakiwezi kufutika
kiurahisi, kwa hiyo ni vizuri kuchagua maneno ya kutumia", amesema Nikki wa Pili.
Mtazame hapa Nikki wa Pili akifunguka mengine zaidi kuhusu ugomvi baina ya Dongo Janja na Young Dee

No comments