"Ebitoke ananikata stimu" - Ben Pol

Msanii Ben Pol ambaye inasemekana alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mchekeshaji Ebitoke, sasa hivi anaonekana kumuepuka msanii huyo kwa sababu ambazo hazijajulikana kwa haraka, kitendo kinachoonesha kumuumiza kihisia Ebitoke.
"Sasa hivi nipo 'busy' sana kwa sababu nafanya mazoezi ya 'show', lakini kiukweli habari za Ebitoke zinanikata 'stimu' kabisa, 'so' nikitulia naweza nikakucheki", alisikika Ben Pol akimjibu mwandishi wetu.
Wiki iliyopita Ebitoke alikuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, na kulalamika kuwa msanii huyo ambaye alikiri kuwa na hisia naye za kimapenzi sasa hivi hapokei simu zake, na wala hajibu ujumbe mfupi anaomtumia katika simu yake, hivyo akaomba watu wamsaidie kumuuliza Ben Pol, kwa nini amefikia uamuzi huo.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments