SIMBA KUWAVAA NAKURU BILA KIKOSI CHA KWANZA LEO, ITAWAKOSA WACHEZAJI HAWA..
Klabu ya Simba itawakosa wachezaji wake muhimu leo kutokana na majukumu mbali mbali waliyonayo. Simba inatarajia kushuka dimbani majira ya saa 10 kupambana na Nakuru Allstar kutoka Kenya kugombea nafasi ya kutinga nusu fainali ya sportpesa.
Wachezaji ambao watakosekana ni Kichuya, Ndemla, Mkude, Mzamilu na Tshabalala ambao wanatumikia kikosi cha taifa. Pia Mavugo na Juuko Murshid hawapo nchini kutokana na majukumu ya time zao za taifa.
Hivyo Simba italazimika kuwatumia vijana wa kikosi cha pili kuziba nafasi zao. Na wachezaji ambao wemesalia na wanaweza kutumika katika mechi ya leo ni James Kotei, Luizio, Blagnon, Manyika na Moh.
Hivyo mechi hiyo inategemewa kuwa ya kuishindani kutokana na sura mpya ambazo zinaweza kupewa nafasi ya kucheza leo.

No comments