MFANYAKAZI AWAUWA WAFANYAKAZI WENZAKE 5 BAADA YA KUFUKUZWA KAZI
Mfanyakazi mmoja aliyefukuzwa kazi katika kiwanda kimoja nchini Marekani alirudi katika kiwanda hicho alichokuwa akikifanyia kazi na na kuwaua kwa kuwapiga risasi kichwani waliokuwa wafanyakazi wenzake watano (5) kabla ya kujiua.
John Rubet Neumann 45 alikuwa amejihami kwa bunduki na kisu wakati aliingia katika biashara moja karibu na Orlando huko Florida siku ya Jumatatu asubuni
Mwanajeshi huyo wa zamani wa Marekani alifutwa kazi mwezi Aprili, kwa mujibu wa polisi.
Neumann aliyekuwa anaishi peke yake eneo hilo, alijiua wakati polisi walikuwa wanakaribia kuingia katika majengo hayo.
Mamlaka zinasema kuwa hakuwa na leseni ya kumiliki bunduki.
Aliondoka katika jeshi la Marekani mwaka 1999.
No comments