A. T - 'BIFU LA ALI KIBA NA DIAMOND, CHANZO SIO MUZIKI MIMI NAKIJUA CHANZO ILIKUWA MPIRA WA MIGUU'
Msanii A.T leo kupitia kipindi cha XXL cha kituo cha redio cha Clouds fm amefunguka kuhusu kisa cha ugomvi katika ya wasanii Ali kiba na Diamond platnumz.
AT amesema kuwa watu wengi wanaongea tu bila kujua chanzo halisi cha ugomvi wa Diamond na Ali kiba ila yeye ndiye shahidi namba moja kwa tukio.
AT amesema ugomvi wa Diamond na alikiba haukuanzia kwenye muziki kama wengi wanavyojua badala yake ili kuwa kwnye mchezo wa mpira wa mguu.
Msanii @at_original leo alikuwa kwenye #XXL ya #RedioYaWatu ( @cloudsfmtz ) kutambulisha wimbo wake mpya. Wimbo huo ( #KunaNini ?) unazungumza sana kuhusu bifu maarufu ya @diamondplatnumz na @officialalikiba.
Katika maongezi yake, #AT alisema kwamba sababu za ugomvi huo zinazoongelewa mitaani sio za kweli na yeye anafahamu ukweli. #AT anasema ya Mondi na Kiba ilianza 2010 walipokuwa Muscat - Oman
" Walikuwa wanacheza game ( #FIFA ). Diamond alikuwa amemfunga Ali Kiba. Ali akapata 'free - kick ' ( kama angefunga angesawazisha ). Alipotaka kupiga, Diamond akampush. Hapo wakaanza kuzinguana sana na kutaka kupigana. " alisema @at_original.
#AT aliendelea kusimulia kwamba katikati ya ugomvi huo ndipo alimsikia @officialalikiba akisema kwamba kuna vitu @diamondplatnumz anavifanya yeye hajapenda. Jambo hilo lilimfanya #AT afahamu kwamba kuna sababu nyingine nyuma ya ugomvi huo. Alisema kuna vitu #Diamond alikuwa anamfanyia #AliKiba lakini hadi mwisho wa kipindi hakutaja ni vitu gani.
.
" @officialalikiba ni pure artist, @diamondplatnumz ni entertatainer tu. Diamond anaimba 'mass choir' kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya. Ali kiba ni msanii wa kweli ametulia anafanya muziki wake tu " Maneno ya AT kwenye #XXL ya #RedioYaWatu.
" Mimi ni shabiki namba 1 wa @officialalikiba kuliko hata Abdu Kiba. Ila sio kwamba namchukia @diamondplatnumz " 🎤 @at_original.
#AT akibonga ndani ya #XXL wakati wa utambulisho wa kazi yake mpya.

No comments