BAADA YA MIAKA MIWILI JUMA NYOSO AREJEA LIGI KUU.. ATUA TIMU HII.
Amerudi tena, baada ya kutumikia adhabu ya miaka miwili baada ya kufanya vitendo ambavyo haviruhusiwi mchezoni, Juma Nyoso amerejea tena ligi kuu.
Leo klabu ya Kagera sugar imetangaza kumalizana na beki huyo ambaye amepata kukipiga katika klabu za Simba na Mbeya City.
Sambamba na Juma Nyoso, mchezaji mwingine ambaye ametangazwa kusajiliwa na Kagera ni Peter Mwalyanzi ambaye aliachwa na klabu yake ya zamani Simba.
No comments