-->

Header Ads

UTATA WAIBUKA MAN UNITED JUU YA UHAMISHO WA POGBA, FIFA WAOMBA NYARAKA KWA UCHUNGUZI

FIFA wamethibitisha kufanya maombi kuhusu taarifa zaidi za uhamisho wa rekodi ya Dunia wa Paul Pogba kutua Manchester United.

Kiungo huyo wa kimataifa alisajiliwa kwa kiasi cha Pauni milioni 89.3 (€105.2m) Agosti 2016 kutoka kwa mabingwa wa Serie A , juventus.

Taarifa kutoka kwenye kitabu kinachoitwa ( The Football Leaks: The Dirty Business of Football, )  kilichochapishwa nchini Ujerumani wiki hii kimedai kutoa taarifa zaidi kuhusu dili hilo pamoja na malipo yote ya dili hilo ambapo jana taarifa hiyo iliripotiwa sana na vyombo vya habari mbalimbali.

Hata hivyo FIFA wamesisitiza kwamba hakuna uchunguzi rasmi , wamethibitisha kwamba wanataka kuangalia swala hilo kwa undani kwanza.

Taarifa kutoka FIFA inasema," Tunathibitisha kwamba FIFA/TMS imefanya maombi kuhusu uhamisho. Hatuna maoni yoyote kwa sasa."

Uhamisho wote wote wa kimataifa ni mamlaka ya FIFA, kwahiyo uhamisho wa Pogba mwezi Agosti ulipitishwa na FIFA kwa kutumia utaratibu wao wa ( International Transfer Matching System (TMS).) 

Manchester United wamesisitiza kwamba FIFA wana nyaraka zote za uhamisho wa Pogba tangu ulipokamilika.

Taarifa kutoka Man United inasema," Hatutoi maoni yetu kuhusu mikataba. FIFA wana nyaraka zote tangu kipindi cha uhamisho huo mwezi Agosti."

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA

No comments

Powered by Blogger.