-->

Header Ads

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA WIKI HII, MAHREZ KUTUA ARSENAL HUKU CHELSEA KUMRUDISHA LUKAKU.


Alex Oxlade Chamberlain anavutiwa kufanya kazi na  Jurgen Klopp na ameonyesha kuwa tayari kujiunga na Livepool  endapo tu Arsenal watakuwa tayari Alex kwasasa mkataba wake umebakiza miezi 12 zaidi sawa na mwaka mmoja (Mail Sports)

Maboss wa Chelsea wamejipanga kumalizana na Antonio Conte mapema ili kuongeza mkataba mara baada ya Inter Milan kutajwa kumuwania Kocha Huyo, Conte pia anatarajiwa kupewa dau kubwa kwaajili ya Usajili wa wachezaji (Daily Mirror)

Chelsea wanatarajiwa kuwashawishi Romelu Lukaku Wa Everton , Alexis Sanchez wa Arsenal na Beki wa Southampton Virgil Van Dijk (Daily Mirror)

Manchester United wako tayari kupambana na Chelsea katika kuwania kumsajili Romelu Lukaku kwa kuweka pauni milioni 85 za Kiingereza , Hii ni vita ya Pesa (Daily Star)


Msahau Alvaro Morata kwenda Manchester United na Chelsea mara baada ya taarifa kutoka Gazeti la MARCA kusema kuna Timu ya China inamwitaji kwa pauni milioni 147.

Hatimaye Manchester United wametangaza kumpa nafasi nyingine David De Gea kuongeza mkataba mwingine hii ni baada ya taarifa kuwa kipa huyo anasakwa na rada za Real Madrid (Manchester Evening News )

Mwana Kwata Unit Blog Manchester United wanataka kumsajili Eric Dier mwenye miaka 23 , Gharama zinazotajwa ili kumsajili Beki huyo ni Pauni milioni 40 za Kiingereza, (Daily Mirror)

Riyadh Mahrez anatarajiwa kuondoka Leicester City na kwenda Arsenal , Kupitia The Independent wameandika habari hii, Huku vilabu kama Chelsea na Spurs vikitajwa pia Kumwania M'Algeria huyo.

No comments

Powered by Blogger.