-->

Header Ads

UZURI NA UBAYA WA ULAJI WA UDONGO KWA WAJAWAZITO NA UMBUMBUMBU KWA MTOTO TUMBONI

MADHARA KWA WALA UDONGO
Tumezoea kuona mama mjamzito akila sana udongo japo pia wapo ambao hua wanakula licha ya kuwa si wajawazito. Yawezekana hawa woote wanakula kutokana na hamu ambayo husikia pasipo kujua kuwa madhara yake ni makubwa kushinda hiyo hamu ambayo uwezo wa kuijuia upo chini ya mtumiaji. Nimemeona nifanye upekuzi ili nawe mwenzangu utumiae hii kitu uone faida na hasara za kutumia udongo lakini kwa bahati mbaya kwako mtumiaji faida sijapata zaidi ya hasara ambazo ni---

1.kusababisha mikwaruzo, michubuko na kupata majeraha ya ndani kwenye utumbo.

2.Ugonjwa wenye homa na maumivu makali unaojulikana kama appendicitis ambao tiba yake ni upasuaji.

3. Na pia udongo una uchafu wa kila aina vikiwemo vijidudu vya bakteria na mayai ya minyoo, hivyo kuutumia kama chakula ni hatari kwa afya ya wewe utumiaye…..
zipo hasara nyiiiiiingi ila kwasababu mi nipo kukupatia kiduuuchu,nadhani kwa leo hicho kitakutosha. Ahsante

Udongo ule una kuwa un-sterilized na hivyo uwezekano wa kupata maambuziko ni mkubwa sana.
Baadhi ni minyoo, kuna bacteria (na hatari zaidi ni TB) n.k.

Hatari kubwa zaidi inayoweza kukupeleka pabaya ASAP ni kodole tumbo. Hiki hakitibiwi kwa dawa ila operesheni pale kinapokuwa katika kiwango cha juu. Kama upo KM nyingi na hospital kinaweza kupasuka na hapo RIP inakuwa karibu nawe.

Hata kama kimeondolewa bado madhara ya infections zitokanazo na ulaji ni kubwa !
share kwa wajanja ili nao wapate faida kwani wanawake wanapenda sana kula udongo hasa wajawazito



Wanawake wanaokula udongo wakiwa wajiwazito wamo katika hatari ya kuwafanya watoto watakowajifungua kutofanya vizuri shuleni.


Utafiti uliofanywa na shirika la African Council for Gifted and Talented unaonyesha kuwa watoto ambao kina mama wao walikuwa wakitumia udongo hawamakiniki darasani.

Mkuu wa shirika hilo Profesa Humprey Obora amewaambia wanahabari jijini Nairobi kuwa utafiti huo umefanywa kwa watoto wanaopelekwa katika taasisi hiyo ambayo hujihusisha kutambua na kukuza vipawa vya watoto wakiwa bado wachanga.

Kwa kawaida wanawake wengi hutumia udongo huo baadhi wakidai kuwa wana upungufu wa madini ila wengi wao huzidisha matumizi yake.


Zaidi ya wazazi 4000 walihusishwa katika utafiti huo lakini ni 1000 tu ambao maoni yao yalitumika kuandaa ripoti ya utafiti huo.

Taasisi hiyo ilikuwa ikifuatilia matokeo ya watoto hao wakiwa shuleni kwa muda wa miaka minne na wakatambua kuwa wale ambao hawakuwa imara darasani mama zao walikuwa na historia ya kutumia udongo wakiwa wamebeba mimba zao.

Watafiti hao wanasema kuwa kutokana na hayo ubongo wa watoto waliozaliwa huchelewa kushika mambo.

Wasimamizi wa mradi huo waliwahusisha wazazi kutoka katika sehemu mbalimbali nchini Kenya ambako kuna vituo vya shirika la African Council for Gifted and Talented.

Kadhalika utafiti huo unaonyesha kuwa wanawake katika miaka ya ishirini huwa na hamu kubwa kutumia udongo



JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.