-->

Header Ads

TAARIFA; JONAS MKUDE APATA AJALI NA MASHABIKI WAKITOKEA DODOMA. TAARIFA KAMILI HII HAPA.

Jonas Mkude, kiungo anayechezea klabu ya Simba amepata ajali ya gari ndogo akiwa na mashabiki wengine wengine wa Simba wakitokea Dodoma walikocheza fainali ya Kombe la AZAM.

Ajali hiyo ilisababishwa na kupasuka kwa tairi na kupelekea gari kupoteza mwelekeo na mwishowe kupinduka.

Mkude amekimbizwa hospitali Dar es salaam na majeruhi wengine wakifikishwa hospitali ya Morogoro huku ikiripotiwa mmoja wa abiria aliyetambulika kwa jina la Shoze akipoteza maisha.

AkisiTv inawapa pole waliofikwa na msiba na tunaungana na wapenzi wote wa mpira kuwaombea majeruhi wote.

Endelea kufuatilia AkisiTv kwa taarifa zaidi.

No comments

Powered by Blogger.