-->

Header Ads

LIPUMBA ATIA AIBU KUHUSU IDADI YA WABUNGE CUF



Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa, leo ameacha maswali na sintofahamu ya hali ya juu wakati akijibu maswali kwenye mahojiano na kituo cha television na cha Clouds.

Lipumba alishindwa kujibu ikiwa chama chake cha CUF kina jumla ya wabunge wangapi katika Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.


Lipumba alikua na kigugumizi cha idadi hiyo, akasema ni thelathini na kitu na baadaye kusema 35 idadi ambayo ilikanushwa na takwimu zinazotambulika ambapo mtangazaji wa clouds tv B. KABAYA akamsahihisha kuwa ni idadi ya wabunge 42 wa CUF kwa sasa.

Baadaye lipumba alijitetea kwa kusema idadi aliyoitaja ni ya wabunge waliochaguliwa ila jumla na wale wakuteuliwa ndio wanafika arobaini na kitu..

No comments

Powered by Blogger.