-->

Header Ads

HII NDIO LAANA YA KUWA NA VIPAJI VINGI NA UWEZO MKUBWA

Duniani kote watu wenye uwezo mkubwa na kipaji katika mambo fulani wanapewa heshima kubwa sana. Vipaji huwafanya baadhi ya watu kuishi katika dunia yao wenyewe ambayo kwa kikubwa ni ile ile dunia ambayo wanaodhani hawana vipaji wanaitamani.

Lakini, kwa kiasi fulani kuwa na vipaji pamoja na uwezo mkubwa inaweza kuwa laana; usishangae sana nitaeleza.

Mtu mwenye vipaji vingi yuko katika hatari kubwa ya kutosonga mbele, ana vitu vingi akilini kiasi kwamba inakua vigumu wakati mwingine kuamua ni kipi aanze nacho na kipi amalizie. Watu wenye vipaji hasa zaidi ya moja wana chaguzi nyingi ambazo wanaweza kufanya, wanajiamini kuwa watafanikiwa kutokana na uwezo mkubwa walionao.

Watu hawa bila kudhamiria hujikuta wako “comfortable” na hatua waliyofikia kwenye maisha wakiamini kuwa chochote wanachohitaji hakitawatoa jasho kama wengine bali watafanikisha kwa urahisi sana.

Vipaji vingi huchanganya, mtu anapokuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi kuna mfululizo wa kusita sita na wakati mwingine watu wa namna hii hawatulii na jambo moja; wana kasumba ya kugusa kila ambacho wana uwezo wa kufanya na kukiacha.

Kwa kawaida, kutokana na uwezo mkubwa wa akili zao ni rahisi sana kwako kuboreka na shughuli moja; wakifanya jambo kwa muda huizoea na kuondoa changamoto ambayo huwapa furaha ya kuifanya kazi hiyo.

Vipaji vingi sio laana kwa wote bali kwa baadhi ya watu, kuna wenye vipaji vingi ambao wamefanikiwa kuvitumia vipaji vyao kwa mafanikio makubwa; hata hivyo inahitaji utulivu wa hali ya juu katika kuelekeza akili na nguvu kufanya yale ambayo yanaweza kuwafikisha kwenye mafanikio.

Wenye vipaji vichache mara zote wanajua hawana akiba ya kuringia hivyo mara nyingi hujitahidi kutumia kile kidogo walichonacho kuhakikisha wanafikia wanapotaka kwenye maisha.

Tukichukulia tasnia ya muziki Tanzania, Diamond ni msanii mwenye mafanikio kwa sasa kuliko msanii yeyote Yule nchini lakini swali ni je, Diamond ndiye mwenye kipaji kuliko wote?? Ukiangalia kwa undani utagundua kuna wasanii wengi tu wenye VIPAJI zaidi ya Diamond, wanaoimba na kuandika vizuri zaidi yake, wana vipaji vingine vingi nje ya muziki pia lakini hawafikii hata robo ya mafanikio aliyonayo Nassib Abdul “Diamond”.

 Hii inatupa picha kwamba mafanikio hayaji kutokana na kile ulichonacho, uwezo na vipaji vyako bali mafanikio huja kwa wewe kuchukua hatua na kupambana.

Hata kama una vipaji 1000, inakubidi uvifanyie kazi kama mtu ambaye ana kipaji kimoja pekee. Pigana sana kama vile hauna kipaji.

 JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA

 Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.