DONALD TRUMP HAYUKO SALAMA.
Alipotangaza nia ya kugombea urais wa taifa kubwa duniani watu wengi waliamini anatania, taratibu akaendelea kupenya hadi alipochaguliwa na kuapishwa rasmi kuwa rais wa 45 wa Marekani hapo Januari 20,2017.
Donald J. Trump huenda ni mtu anayetaniwa sana na vyombo vya habari na wachekeshaji wengi nchini mwake, amekosolewa sana sera zake. Rais huyo na timu yake wamekacha sherehe za White House Correspondent Dinner zilizofanyika usiku wa kuamkia leo lakini hiyo haikusaidia kuacha kuongelewa na kupondwa na Hassan Minhaj ambaye alisheheresha usiku huo.
White House Correspondence Dinner ni utamaduni wa rais na watu wengine ndani ya White House kukutana na waandishi wa habari wanaofanya kazi ya kumripoti rais na yanayoendelea ndani ya ikulu ya Marekani; utamaduni huu ulianzishwa mwaka 1914.
Hassan ambaye ni mfanyakazi wa kituo cha Comedy Central, alianza hotuba yake kwa kuongelea jinsi kazi zisizokuwa na watu; kazi ambazo Wamarekani hawawezi kufanya ndizo zinadondoka mikononi mwa wahamiaji akitolea mfano wa kazi yake ya usiku huo.
Minhaj pia, aliponda vyombo mbalimbali vya habari kikiwemo kituo pendwa cha Donald Trump; FOX.Mara kwa mara Trump amavituhumu vyombo vya habari kwa kumripoti vibaya na kituo pekee anachokiamini ni FOX.
Unaweza kutazama na kusikia kila alichosema Hassan Minhaj hapa chini.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA
Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments