SIPANGIWI CHA KUPOSTI
Rafiki
kipenzi jibu, siasa imekukoma
Mume wako si
nasibu, lini utaitwa mama
Punguza
hiyo gadhabu, mwenzio bado nasoma
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
Punguzeni
kunihoji, mi sijui kuandika
Mpaka penzi
unafoji, unabaki tu kudeka
Uza hata
mafuriji, hutokuja kuteseka
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
Ujue
nakutegemea, sikuonana na malima
Sitaki
kuchechemea, babu yangu mkulima
Mwana
ukimkemea, kesho nitakuja mama
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
Chipsi kavu
maandazi, kula na juisi mende
Ukishiba we
jambazi, ongezea na makande
Kisha piga
na miluzi,shusha bakuli udende
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
Ukiona
inakukifu, kaoge barabarani
Kisha keti
kwe sakafu, weka simu sikioni
Katakata na
mkufu, jivike kiuononi
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
Kamoni
nimepotoka!, eti posta iko wapi?
Ninataka
kuokoka, kwa majuma mangapi
Jana
nilivyokusuka, ulisahau kipatupi
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
Deshi deshi
mchumbako, aka kasemo buana
Dalili za mchepuko,
kamenenwa sanasana
Ni enzi za
nyuma huko, hasa kitaka semana
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
Nipe moja
basi bana, leo mwenzio mgonjwa
Na Sitaki
kushikana, ila ntajaribu kunywa
Pombe
zenyewe za jana, hata damu nitanyonywa
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
Sitamani cha
mwenzio, kama chako ukitunzi
Unakimbio
kwa mbio, kumbe hujui mapenzi
Anzia kwenye
sikio, shuka mpaka kwa nazi
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
Umelewa nini
hapa, mwenyewe sijaelewa
Ila
ninatupatupa, maneno kwenye behewa
Ha ha ha ha
ha ha kapa, mimacho limekodowa
Sipangiwi
cha kuposti, naandika nisojua
No comments