WAZIRI TIZEBA: Siko kwenye nafasi ya Kutangaza Njaa lakini Nisingemshauri Rais kufanya hivyo
Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba akizungumza na mmoja kati ya
wafanyabishara leo katika kongamano la baraza la nafaka Afrika mashariki
Dar es salaam. Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles
Tizeba amesema hatakuwa na sababu ya kuendelea kuwa waziri endapo
Watanzania watakosa ugali juu ya meza.
Dk Tizeba amesema hayo leo Alhamisi wakati wa mkutano wa saba wa baraza la nafaka la ukanda wa Afrika Mashariki (EAGC).
Amesema Serikali itaendelea na jukumu la kuhakikisha chakula kinakuwepo nchini.
Waziri
amesema mwanzoni mwa mwaka huu baadhi ya wabunge na vyombo vya habari
vilimshinikiza atangaze uwepo wa njaa nchini lakini hakufanya hivyo kwa
sababu hapakuwa na njaa.
"Siko kwenye nafasi ya
kutangaza njaa lakini nisingemshauri Rais kufanya hivyo kwa kuwa licha
ya mavuno kidogo yaliyokuwepo kipindi kile, Serikali inaamini watu
walikuwa na chakula cha kutosha," amesema Dk Tizeba.
Amesema
hata yeye angekuwa Rais asingeweza kutangaza njaa kwa kuwa hali hiyo
ilitokea ikiwa ni miezi miwili tu tangu wafanyabiashara waishinikize
Serikali kutoa vibali vya kuuza nafaka nje ya nchi.
"Isingewezekana
njaa kuja ghafla. Kitendo cha wafanyabiashara kutaka ruksa ya kuuza
mazao nje kilimaanisha chakula kilikuwepo cha ziada," amesema Dk Tizeba.
Hata hivyo, Dk Tizeba amesema hali ya chakula kwa mwaka huu imepungua kwa asilimia tatu kulinganisha na mwaka jana.
Kutokana na hilo, amesema chakula kinapaswa kutumika vizuri kuepuka upungufu.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,