Vanessa Mdee Kesho kuwaongoza wasanii wengine Kwenye
MREMBO anayefanya poa katika tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee kesho Jumapili atakua na kibarua cha kuwaongoza wasanii wenzake katika Tamasha la Fiesta 2017 litakalofanyika kwenye Uwanja wa Samora, Iringa. Hiyo ni baada ya jana Ijumaa kufanya tamasha hilo kwenye Uwanja wa Sabasaba uliopo Njombe.
Mratibu wa tamasha hilo, Fauzia Abdi aliitaja listi ya wasanii wengine watakaokinukisha Samora kuwa ni; Joh Makini, Roma, Maua Sama, Nandy, Jux, Ben Pol, Chegge, Aslay, Blue, Stamina, Madee na Darassa na wengineo kibao.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments