-->

Header Ads

KISIWA CHA ZUNIGA (7)

 

Na Adalgisa Kweka.

Alipozinduka alijikuta kwenye kichumba chenye hewa Nzito kikiwa na nyasi kwa chini hakikuwa na kitanda wala kitu kingine chochote. Alianza kuinuka huku aketi,miguu yake ilikuwa inamuuma sana alipoiangalia aliiona imevimba hali ile ilimshtusha kwani haijawahi mtokea kabisa.aliwaza wazawa wale wamempa nini mpaka kupelekea miguu yake kuvimba kiasi hicho hakupata jibu.
"we-wee"alisikia mtu akiita alipoangalia mbele alikutana na chumba kingine kikimuangalia kutokana na mwanga mkali kwenye mahabusu hiyo ambayo Tuli hakuitambua, aliweza kuiona sura ya mtu iliyofurika damu nakumfanya asitambulike ni mtu gani ijapokuwa sauti iligundulisha jinsia yake ni Yakiume. Tuli alijiburuza licha ya nyasi zile kumletea hali ya kuwasha ambapo alipojikuna alivimba,shida yake ilikuwa afike hadi kwenye nondo za chumba chake iliaweze kuongea na mwenzake huyo, hakumuwaza yule mjamzito wala saluat.
"wewe"alimuita kwa sauti ya chini sana huku akiangalia huku na kule ambapo aliona vyumba ni vingi Sana pande zote mbili alihisi chumba chake kiko katikati, ijapokuwa hakujua kama vyote vilikuwa na wafungwa zaidi ya cha mbele yake hii nikutokana nakukosa uwazi sehemu za pembeni ila kwa hili mkandarasi alistahili pongezi.
"nd-i-y--o"aliitikia taratibu kudhihirisha hakuwa na nguvu pia alikuwa na maumivu makali Sana.
"vyumba vyote vina watu" aliuliza kwani alitaka kuliua dukuduku lake.
"hapana baa--d--hi"
"umefanya nin mbona uko huku" hili ndo lilikuwa swali la muhimu kuliko yote ijapokuwa kila swali unalouliza kisiwani hapo linaumuhimu. Yule kijana alikuwa kimya kwa Muda, Tuli akajua hili swali aliwezi jibiwa kutokana na sharia za kisiwa cha Zuniga.
"niliua" hatimaye alijibu lakini jibu lake lilikuwa ganzi kwenye moyo wa Tuli ambaye alibaki anamshangaa kijana mwenziye ni kwa namna gani aliweza kuua, kwanza alimuua nani?,alishasahau kuwa na yeye yupo mahabusu kwa kosa hilohilo.
"ndyo niliua, ndo walivyoniambia lakini wao walimuua kipenzi changu Lisa" alikuwa analia machozi yake yalilainisha damu zilizoganda nakutua kama tone moja hakuna aliyeweza kuliona tone lile. Tuli hakuelewa chochote, mambo ya mpenzi ndo hayakumuingia kichwani kabisa. "alikuwa na mchumba kisiwani? Walikutana wapi? Kwanini Lisa alikuwa"yalikuwa mawazo ya Tuli.
"wazawa walimuua Li-sa?"alishapata swali aliuliza kana kwamba anamjua huyo lisa.
"ndyo!! Lisa wangu alikuwa na katoto tumboni, nilikuwa niitwe baba ilikuwa ni Lazima, tukapanga kutoroka licha ya ugumu wote lakini hawakuruhusu litokee wakamua Lisa wangu baada ya lile pamba-no, mimi sikumuua yule -"
"shshhshh"ilikuwa ni sauti iliyotoka chumba kingine ikiwasihi wanyamaze, wote walitii amri kwani walijua fika mzawa anakuja.
"MIMI SIKUMUUA MZAWA" yule kijana alianza kupayuka kitendo kilichowashtua wengine.
"shshhshh..." "we Mzawa""...mwambieni anyamaze "zilikuwa ni baadhi za sauti za minong'ono kutoka kwa wafungwa wenzie wakimhimiza anyamaze lakini hakusikia la mtu, alionekana kuchoshwa na maisha kiasi chakuamua afe.
"shshhshh wewe ni mpiganaji" baada ya wengine kuongea Tuli naye alisema ya moyoni,hakutaka afe kwani aliamini hata lisa asingependa kumuona mwanaume anayempenda anakufa kwa kuamua. Roho ya kifo ilishamkaba bado aliendelea kuropoka, Tuli alijivuta taratibu kurudi alipokuwa mwanzoni alijifanya amelala kwani alishasikia sauti ya mzawa ikiita wazawa wengine ghafla taswira ya marehemu Joe Shabibu ilimrudia aliziona sura za wazawa wale zikimsubiria akate roho, taswira hiyo ilimfanya Tuli akubaliane na mawazo mpenziwe Lisa.
"wazawaaa!!"Alita mzawa yule dakika si chache walifika nakuanza kuelekea chumba ambacho sauti ilikuwa ikitokea.
"Mtatua tu hiyo ndo hukumu yetu mmetuchukua mje mtumie nguvu yetu kutengeneza nchi mpya! Mje muwatesa wazazi wetu! Ndugu zetu! Jamii zetu! Bora kufa mapema kuliko kuteseka na kufa baadaye"
"WAZAWA NYWALEE!!"ilikuwa ni amri ambayo hakuna aliyeielewa zaidi ya wazawa wenyewe lakini chaajabu baada ya amri Ile vishindo vikubwa vilisikika vilivyoashiria Kuwa wazawa walikuwa wanakimbia sikutembea tena
"wafungwa wenzangu! aliyetuleta huku si mwingine bali ni RAISI WE-"ulisikika mlio wa risasi ukafuatiwa na kishindo kikubwa kilichoashiria kitu kudondoka walioko mule ndani walishajua ni nini.
"WENYEJII INUKA" mzawa aliyekuwa anaongoza wenzie alitoa amri kwa wafungwa ndani ya mahabusu.
"NDIYO MZAWA"wote waliitikia nakuinuka ila Tuli alibaki amelala huku akisikiliza kinachofuatia hakujua kama mchezo huo ulikuwa na mwisho mzuri.
"Ee Mungu naomba unisaidie nawe Lisa niombee kwa Mola aniepushe na yajayo, Mungu wangu nisaidie" Tuli alikuwa akisali akirudiarudia mara tatu alimuomba marehemu Lisa amsaidie kwakweli alikuwa amechanganyikiwa.
"WAZAWA!"
"MZAWA!"waliitikia
"SIRI YA KISIWA HAIPASWI KUJULIKANA, IKIJULIKANA ADHABU NI!"
"KIFO" waliitikia, papo hapo milio ya risasi ilisikika huku kelele za watu zikisikika kuashiria wamepatwa na risasi hizo, ilikuwa kama vita Kati ya njaa na binadamu. Milio ya risasiiliendelea kusikika huku na kule huku vishindo vya wazawa vikisogea taratibu, Tuli alikuwa akiendelea na sala yake huku akitoa ahadi kemkem kwa Mungu endapo kifo kitampita.
"Mzawa Kuna mfungwa mmoja amelala" sauti ile ilitokea sehemu ya chumba cha Tuli ambaye bado aliendelea na Sala yake.
"Na hapa pia yupo mwingine amelala tena anakoroma"kilikuwa ni chumba mbele ya Tuli.
"HAKIKISHENI KAMA WAMELALA NAKUJA" Alianza kutembea kuelekea kwenye vyumba hivyo. Wazawa wale waliingia chumba cha pembeni ya Tuli ambapo walianza kumgusa mwenyeji yule ambaye alianza kuweweseka akigeuka huku na huku, akiibana miguu yake na kama haitoshi aliishikilia kwa nguvu huku akilia, Muda wote huo mzawa yule kiongozi alikuwa ameshafika pale naye akishuhudia yote.
"Mjomba usinifanyie hivyo, Mjomba nisamehe!" alikuwa analia sana.
"wazawa muamsheni" alikereka na alichokisikia. Wazawa wale walimtingisha mwenyeji yule ambaye alishtuka nakumkumbatia mzawa mmoja wapo.
"mzawa mpelekeni Mkuu wa Kitengo cha Afya" alitoa amri Kisha walimchukua mwenyeji yule nakuondoka naye huku wengine wakibaki kwaajili ya kwenda kwa Tuli,Muda wote huo Tuli aliyasikia yaliyojiri ila hakuacha kusali hata kidogo.
"Mwingine yupo wapi?" aliuliza kiongozi wao.
"Chumba kinachofuata" walitangulia kuongoza njia, walipofika walifungua nakuingia ndani.
"Mbona analala kwenye nyasi?" aliuliza kiongozi yule kwani ni mfungwa mmoja aliyekuwa analala kwenye nyasi ambaye walishamuua tiyari.
"Ana kesi yakuua" alijibu mzawa mmoja ambaye alionekana kuwepo siku yakukamatwa kwake.
"MUAMSHENI!!" alitoa amri. Wazawa wale walimgusa Tuli nakumtikisa Kisha aliamka, Kisha akaanza kulia huku akiifumba mikono yake miwili jambo lililowashtua wazawa wale.
"SIKUMUUA, SIKUMUUA ALINIOMBA DAWA NIKAKATAA SIKUMUUA MIMI"alikuwa kama mtoto mdogo,macho yake yalikuwa yamevimba kutokana nakulia Jana. Akiwa anajitete ghafla miguu yake ilianza kuvuta, Tuli alisahau kuhusu igizo Lake dogo nakuishikiria miguu yake nakuanza kulia.
"miguu yanguu" alipaaza sauti huku kilio kikiisindikiza sauti.
"anatania huyo kiongozi" alisema mzawa yulee. Kiongozi yule WA wale wazawa alikuwa amechuchumaa chini,macho yake yalihamia kwenye miguu ya tuli ambayo licha yakuvaa suruali ilionekana ikiwa imebadirika rangi nakuwa na rangi nyekundu kwenye kwato, kiongozi yule alimpandisha suruali Ile juu kidogo ili aione miguu ile ilivyo kwa juu aliiona imevimba sana na siyeye tu hata wale wazawa walishuhudia pia nakujua kuwa hakuwa akijifanyisha kama alivyosema mwenzao.
"mzawa tumpeleke kitengo cha afya" aliuliza mzawa mmoja kwani kila kitu kisiwani kilienda kwa amri.
"subiri kwanza (alitoa amri) unaitwa Nani?" alimuuliza Tuli Jina lake.
"Tu-li" alumjibu kwa uchungu akijikaza licha ya maumivu kumtesa.
"Tuli umesikia nini?"alimuuliza alihitaji kujua kama Tuli amesikia chochote.
"wameniita muuaji ila siku-muua, miguu yangu" alichanganya mambo huku akilia kutokana na maumivu ya miguu Yake.
"MUWAISHENI KITENGO CHA AFYA HARAKA" amri ilitolewa, Tuli alibebwa na wazawa wale robo saa alishafikishwa kwa mkuu wa kitengo cha afya ambapo kulikuwa na kitanda, walipoingia ofisini walimlaza kwenye kitanda hiko,Tuli aliendelea kulia.
"mnaweza kwenda"
"Sawa mkuu" waliondoka zao. Mkuu yule alisogea mahali alipo Tuli Kisha alimgusa na mkono wake kichwani, Tuli aliona hiyo ndo nafasi pekee aliyonayo yakutumiza matakwa yake, aliuinua mkono wake nakuuishika mkono wa Mkuu kitendo kilichomshtua hata Mkuu mwenyewe.
"Mkuu nakuomba unichome sindano ya usingi-zi maumivu maka-li"alikuwa akilia kuthibitisha alivyojisikia.
"Tuli, nilikuambiaje" kauli ya mkuu yule ilimshtua Tuli kiasi chakumfanya ainue shingo yake kumuangalia kama anamfahamu, alipoinua shingo yake kwa shida alikutana na sura ya mzawa aliyemsajili kwenye kitengo cha afya, mzawa huyohuyo aliyemziba macho usiku wa kwanza kisiwani. Aliyakumbuka vizuri maneno yake aliyomwambia siku ya usajili.
"sikuamka usiku" alimjibuu
"Bali uliongea na mjamzito" alihamia kwenye Mada husika. Alishangaa Mkuu alijuaje akakumbuka alivyomuuliza mjamzito kuhusu kurekodiwa akapata jibu, akajua kwamba atakuwa alimuona tu kwenye kompyuta ila hakusikia chochote hivyo hakuwa na hofu. Alisahau kuhusu maumivu ya miguu.
"SIKUMUUA" alisisitiza.
"Ila ulimuelekeza dawa za aina gani"alisema mkuu
"NOO!(HAPANA!!)".................ITAENDELEA.(kwa maoni Zaidi piga 0679488502)









No comments

Powered by Blogger.