-->

Header Ads

ESTER BULAYA Amvaa Waziri Nchemba


Mbunge wa Bunda Mjini Kupitia CHADEMA, Ester Amos Bulaya, amemtaka Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba, kuwataja watu wanaofanya uhalifu ikiwepo kuwatishia maisha baadhi ya viongozi hapa nchini ikiwepo Nape Nnauye kwani anawajua.

Bulaya ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, na kusema kwamba Waziri anawajua watu hao lakini anaogopa kuwataja kwa kulinda kitumbua chake kuingia mchanga.

Ester Bulaya ameendelea kusema kwamba kitendo hicho sio kizuri kwani kinaweza kutokea kwa watu wengine ikiwemo familia yake, na hivyo atashindwa kuchukua hatua kama ambavyo anafanya sasa.




JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
Powered by Blogger.