Diamond afikishwa mahakamani kwa matunzo ya mtoto
Dar es Salaam.
Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.
Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.
Wito
huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mobeto, Abdullah Zulu na
Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.
Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.
Wakili
Zulu akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi amesema mteja wao Hamisa
Mobeto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke
matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.
“Baada ya kuona
kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto (The
Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito
na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.
Zulu amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,