Matokeo yote Ligi ya Mabingwa UEFA Jumanne
MATOKEO: APOEL 0-3 TOTTENHAM HOTSPUT
Harry Kane amekuwa mchezaji wa saba wa Kiingereza kufunga hat-trick kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa katika mechi ya Jumanne waliyocheza dhidi ya APOEL Nicosia.
Mshambuliaji huyo wa Tottenham Hotspur aliifungia timu yake magoli katika ushindi huo wa Cyprus, akiweka kimiani kwa kila mguu na moja la kichwa.
Kane, 24, sasa amefikia mafanikio ya Waingereza wenzake Andrew Cole, Michael Owen, Wayne Rooney, Alan Shearer, Danny Welbeck na Mike Newell.
MATOKEO: MONACO 0-3 PORTO
Monaco
wameangukia pua mikononi mwa Porto kwa kichapo cha 3-0 katika mechi ya
Jumanne usiku Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye uwanja wa Stade Louis II.
Wenyeji hao walikuwa wa kwanza kuanza kuleta balaa langoni mwa Porto Radamel Falcao akijaribu kufunga ikiwa ni dakika ya nne tangu mchezo uanze.
Porto walipata goli lao la kwanza dakika ya 31 Vincent Aboubakar alipovuta shuti kali lililomshinda Diego Benaglio ambaye aliokoa michomo mingi.
Goli la pili kwa wageni hao lilipatikana dakika ya 69 pale Moussa Marega alipompa pasi nzuri Aboubakar ambaye aliunganisha moja kwa moja hadi wavuni Porto wakiandika bao la pili.
Kikosi cha Sergio Conceicao kiliongeza goli la tatu dakika moja kabla ya mechi kumalizika Marega alipomchongea pasi matata Miguel Layun aliyetokea benchi na kumaliza mchezo kwa ushindi wa mabao matatu.
MATOKEO: SPARTAK MOSCOW 1-1 LIVERPOOL
Liverpool
wameendelea kusubirishwa kupata ushindi wa kwanza Ligi ya Mabingwa
msimu huu baada ya kushikiliwa kwa sare ya 1-1 dhidi ya Spartak Moscow.
Walikuwa wenyeji walioanza kupata goli la kuongoza kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na Fernando, lakini pia Liverpool nao walishindwa kumiliki mpira vizuri na kutengeneza nafasi.
Philippe Coutinho aliisawazishia Liverpool, lakini hawakuweza kuongeza goli la pili na wakapteza pointi mbili tena kwenye kundi E baada ya kushikiliwa kwa sare na Sevilla mechi iliyopita.
MATOKEO: BORUSSIA DORTMUND 1-3 REAL MADRID
Gareth Bale alifungua ukurasa wa mabao akiifungia Real Madrid katika uwanja wa Signal Iduna Park kabla ya Ronaldo kufunga mara mbili.
Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amewajibu vidomo-domo huku akiwashangaza kwa kiwango safi.
Mabao mawili ya Ronaldo yaliisaidia Madrid kushinda 3-1 dhidi ya Borussia Dortmund kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne.
Nyota huyo hajarudi vizuri kwenye mechi za Ligi, kwani hajafanikiwa kufunga kwenye mechi mbili za La Liga tangu amalize adhabu yake.
No comments