ALI KIBA: Najivunia kuwa Mswahili, Wanaigeria wanaimba ngoma zangu mimi..
Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na
wimbo wake 'Seduce me' amefunguka na kusema kuwa lugha ya Kiswahili si
kikwazo kwake na muziki wake kufika kimataifa na kusema yeye anajivunia
kutumia lugha hiyo ambayo kwa sasa ni kati ya lugha kubwa duniani.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
Alikiba
alisema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz wiki kadhaa
zilizopita na kusema anajisikia fahari kutumia lugha ya Kiswahili katika
muziki wake na kusema kufanya hivyo inasaidia pia kukuza lugha yetu ya
Kiswahili ulimwenguni.
"Hakuna kizuizi cha lugha
kwenye muziki zamani tulikuwa tunapenda miziki ya Kiringala lakini
tulikuwa hatujui nini wanaimba, tulikuwa tunapenda miziki kutoka Congo
lakini hatuelewi wanaimba nini na bado mpaka sasa kuna watu wanapenda
miziki ya kizungu lakini hawaelewi kizungu hivyo hakuna kizuizi cha
lugha kwenye muziki. Kiswahili ni lugha kubwa Afrika na ni lugha ambayo
inaheshimika sana barani Afrika na tunapoendelea kuimba Kiswahili
tunaikuza lugha yetu kwanza mimi najivunia kuwa Mswahili nasaidia kukuza
lugha yetu ya Kiswahili ifike kote inapotakiwa kufika kwa sababu tayari
ni lugha kubwa duniani" alisema Alikiba
Aidha Alikiba aliendelea kusema kuwa kwa sasa sehemu ambazo anakwenda
kufanya matamasha yake nje ya Tanzania mashabiki wamekuwa wakiimba
nyimbo zake hizo japo si kwa kupatia lakini ni hatua kuwa wanapenda
anachoimba licha ya kutoelewa maana yake na kudai hiyo ni njia moja wapo
ya kuzidi kukuza lugha ya Kiswahili.
"Kuimba Kiswahili
hakukwamishi kabisa muziki wetu kufika mbali kinachotakiwa kufanya
muziki mzuri tu, mimi nishafanya matamasha mbalimbali nje ya Tanzania
mfano Finland sikuwaimbia tu wabongo au Wakenya, nishafanya matamasha
Oman na sehemu zingine watu wanaimba wewe hawajali yaani, Wanaigeria
wanaimba ngoma zangu mimi, wanaimba japo hawapatii kabisaa lakini
wanahisi nimeimba vizuri ndiyo maana wanapenda na kuimba na mimi" alisema Alikiba
Itazame hapa video ya Alikiba "Seduce Me"JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments